EPL : Je, Southampton atachomoka kwa Chelsea? Liverpool uso kwa uso na Everton

Shadida Salum

Journalist at JamiiForums
Joined
Sep 11, 2020
Posts
69
Reaction score
105


Baada ya kuuanza mwezi Februari kwa kichapo kizito cha goli 9-0 kutoka kwa Manchester United na kisha kupigwa tena 3-2 na Newcastle kwenye michezo ya ligi, Southampton hii leo inashuka tena dimbani kupepetana na Chelsea

The Blues itakayokuwa ugenini leo imepewa imani kubwa ya kushinda mchezo huo, imeshinda michezo 5 kati ya 6 tangu Tomas Tuchel asaini kandarasi ya kukinoa kikosi hicho cha Darajani

Mchezo mwingine ni Merseyside derby ambapo Liverpool inakutana na Everton katika Dimba la Anfield. Mara ya mwisho Everton kushinda Anfield ni mwaka 1999 na mara ya mwisho kushinda Derby hiyo ni mwaka 2010.

Liverpool itatakiwa kushinda mchezo huo na kuomba Chelsea ifungwe ili aweze kurejea katika nafasi nne za juu

Michezo mingine ni kati ya Burnley ambayo itakuwa nyumbani kuumana na West Brom, huku Fulham ikiwa mwenyeji wa Sheffield United.
 
Huyo Southampton atachezea za kutosha, kwa Everton sina shaka kabisa..leo Liverpool ana kazi ya kufanya..
Hao takataka wengine hatuna khabari nao.
#CFC [emoji170][emoji170][emoji170]

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…