Epuka gharama za kumwagilia kwa kutumia mafuta kwa kununua mfumo huu

mushongokle

Member
Joined
Sep 23, 2014
Posts
95
Reaction score
113
Jina la kampuni - Simusolar.

Simusolar inauzwa mfumo wa umwagiliaji. Unatumia Solar Power kutoka katika vyanzo vyako mbalimbali vya maji.

Mfumo huu unakusaidia wewe mkulima kuepuka gharama za mafuta katika uendeshaji. Mfumo huu una uwezo kutatua changamoto ya umwagiliaji kwa mkulima mdogo na mkubwa.

Mfumo huu unaweza kumwagilia kuanzia heka moja mpaka heka 8.

 
Taarifa nzuri, lakini unaandika kama unakimbizwa! weka mfumo, weka bei, weka madaraja ya mifumo na bei ya kila moja!
 
Taarifa nzuri, lakini unaandika kama unakimbizwa! weka mfumo, weka bei, weka madaraja ya mifumo na bei ya kila moja!
Kweli mkuu ni kama kaleta habari za kufikirika lakini haziko katika uhalisia
 
Okay. Kila moja wapo ina sifa tofauti na uwezo wa kumwagilia tofauti kulingana na Watt.

Aina ya kwanza ina uwezo wa kumwagilia lita 1000 kwa saa.
Ya Pili ina uwezo wa kumwagilia lita 2000 kwa saa.
Ya tatu ina uwezo wa kumwagilia lita 2300 kwa saa.
Ya nne ina uwezo wa kumwagilia lita 2400 kwa saa.
Ya tano ina uwezo wa kumwagilia lita 10000 kwa saa.

Pindi mteja akihitaji, watu wa kampuni wataenda shambani kwake kwa ajili ya ushauri na price.
 
Mkuu uzi wako uweke vizuri iwe kama kweli kuna biashara... Mana tangu kichwa cha habari na kila sentensi ndani ya habari havina ushirikiano baina yao.

Mpaka umenifanya nirejee post zako za myuma kutazama uandishi wako wa nyuzi!


Project yako inaonekana ni nzuri sana hasa kwa kilimo cha kisasa, basi tueleweshe vizuri tuchangamkie fursa mkuu.


Mambo kama ayo husindikizwa na angalau kapicha ili kuonesha uhalisia na kuteka hisia za wasomaji kwaajili ya biashara.

TUMWAGIE MPUNGA MKUU
 

Nipe simu za wakala wenu aliyeko Dar es Salaam, au ofisi zenu ziko wapi hapa Dsm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…