Epuka hili, tafadhali

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
5,771
Reaction score
14,732
Jamaa mmoja alifungua duka basi marafiki zake, familia, na majirani walinunua bidhaa kwake na wengine wakikopa, Baada ya miaka kadhaa, hiki ndicho kilichosalia.

Mara nyingine tunakubali ndio wakati tungepaswa kusema hapana. Unakubali ndio ukifikiria unawasaidia watu lakini kwa kweli unapoteza na kutoa kazi ngumu na kujitolea kwako, halafu kila mtu anakugeuka.

Usiseme ndio kila wakati.

Wekeza katika biashara yako na uokoe, kuwa mwerevu, usiruhusu kila kitu kupotea. Kwa njia hii, unaweza kuepuka kukutana na hali kama hii.
 
Kuna jamaa nilimpa ushauri huu baada ya kupata compensation ya mama yake aliegongwa na Gari kwenye zebra crossing
Alipata hela nyingi sana wakagawana ndugu wa3 yeye akaamua kufungua mini supermarket
Nikaliona duka nikamtahadharisha usikope mtu
Baada ya miaka 2 tu hana duka wala ndugu
 
Ukiwa unaguswa na kila story ya huzuni ya watu wanaokuja kulia shida kwako, mwishowe na wewe utatusimulia story yako ya huzuni na ya kusisimua.
 
Aisee kumbe sio duka tu lililopukutika, hadi mmiliki kapukutika.
 
Hiki ndio kilinikosanisha na ndugu. Wanaona biashara inashamiri, wakaona shida zetu zimeisha, kila simu ni kuomba msaada, unawaambia sina hela mshahara wangu mdogo. Akikata simu anapiga kwa mama analalamika Boban anabishara nzuri lakini kila ukimuomba msaada anasema hana.
Kwenye kikao kimoja nikawauliza...mnataka tuwe tunagawana faida ya biashara? Nikifilisika mnicheke?
 
Kwahiyo kazi ya "uwasibu" ina mshahara mdogo sana mpaka ukaamua kujiajiri
 
Sio kukopesha tu duka, hata wanaume wenye vipato na ajira nzuri, asipo kuwa makini, kichwa cha chini na umalaya asipodhibiti unakufilisi kabisa
 
Jamaa mpk kabaki mifupa, kuweni na mipaka. Hata ndugu hugeuka maadui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…