Kadiri uwezavyo nakushauri kijana epuka sana kuchora tatoo katika mwili wako. Kuna mambo mengi yamejificha nyuma ya uchoraji wa tatoo katika mwili wa binadamu. Tatoo hata kama unachora tatoo ya msalaba au kitu unachofikiri ni kitakatifu, ulichofanya ni kitu kibaya na hakitakuacha salama. Tatoo zote ni alama au lugha inayowakilisha jambo fulani katika ulimwengu wa giza. Tatoo ni signature za shetani mwilini mwako. Epuka kuchora tatoo kwa gharama yoyote ile!