Epuka kasumba ya "Eneo lenye mzunguko mkubwa"

Financial Analyst

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2017
Posts
1,849
Reaction score
3,506
Sipingani kuwa, idadi kubwa ya watu katika sehemu inaweza kuongeza demand ya bidhaa au huduma.

Lakini je, kweli hiyo "idadi kubwa ya watu" wanahitaji bidhaa au huduma yako unayofikiria kuwafikishia.

Usihangaishwe na ushauri wa watu au imani yako binafsi kuwa sehemu yenye watu wengi ndio suluhisho la kutafuta mafanikio katika biz yako.

Badala yake jitahidi kuyafanyia uchunguzi yafuatayo katika location unayoifikiria:

1. Hali ya kiuchumi na kipato ya watu katika eneo hilo.

2. Je wana "uhitaji" wa bidhaa au huduma yako.?

3. Je hali yao ya kiutamaduni, style ya maisha na dini ni rafiki kwa biashara yako.

4. Je strategy unayotaka kuapply katika ushindani na uhudumiaji wa wateja imeshazoeleka na kutumika kabla.?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha theory zako mkuu, biashara inafanya vyema kwenye mzunguko wawatu mbona mifano madhubuti ipo kariakoo, mbagala rangitatu, buguruni nk, uwezi nambia mimi nifungue biashara ya miamala ya pesa hapa nyumbani eti tupate faida sawa na yule anayeifanya mbagala rangitatu.

Kama unaamini hizo theory zako fungua duka la nguo nyumbani kwako upigwe za uso akili ikae sawa.

Tuache theory za kupotosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujamuelewa vzr.
 
Asante sana mkuu nimekupata vizuri sana kingine cha kuongezea ni hizi locations zenye mzunguko mkubwa kwa muda mfupi mfano machimbo yanayoibuka, kilimo, stand.

Wengi wanafanya uwekezaji mkubwa wa majengo ya biashara za frem/ hotel/guest house/ halafu baada ya muda rasilimali zinakwisha kama vile mererani, geita au stand inahamishwa inabaki hasara ya muda mrefu. Frem iliyokuwa ikipangishwa kwa laki 3 kwa mwezi inakuja kwa mama ntilie elfu 20

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…