Epuka kusambaza Taarifa potoshi kipindi hiki cha uchaguzi, thibitisha mara kwa mara

JamiiCheck

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
245
Reaction score
267
Katika kipindi cha uchaguzi Taarifa za uzushi hutengenezwa kwa kiwango kikubwa na kusambazwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mitandao ya kijamii.

Taarifa hizo zinaweza kuhususisha sauti, video, picha na maandishi mbalimbali huku ikidaiwa kuwa imetolewa na mwanasiasa fulani ama zinamuhusu mwanasiasa fulani.

Thibitisha taarifa unazozitilia mashaka mara kwa mara ili uweze kufanya maamuzi yaliyo sahihi, bila chuki wala woga unaosababishwa na Taarifa potoshi. Tembelea jukwaa la Jamiicheck.com kujifunza mbinu, ama kuwasilisha taarifa mbalimbali unazozitilia mashaka na unahitaji uhalisisa wake.
 
Taharifa kama CCM yapoteza jimbo ukizitoa mapema tutakushughulikia πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Uchaguzi upi wakati tumekubaliana na mzazi wa upande mmoja kwamba hamna uchaguzi?😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…