Epuka makosa haya kwenye maisha.

Epuka makosa haya kwenye maisha.

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Epuka makosa haya kwenye maisha, yatakuchelewesha na yatakuzeesha haraka.

Huyo mimi ndiyo nilimsomesha.

Hilo paa mimi ndiyo nimempaulia ili ahamie kwake, alikwama kabisaaaaa.

Hicho cheo mimi ndiyo nilimfanyia mpango akakipata.

Usimuone hivyo mimi ndiyo nilikuwa nampa nauli sasa hivi hanijui.

Huyo alisomaga kwangu.

Katoka mikoani hajui kuvaa, midela tu kutwa nzima, nimempeleka kwa fundi wangu Sinza sasa anajifanya mjanja kupendeza kunizidi.

Sadaka anaombaga kwangu huyo.

Darasani nilikuwa namburuza hukoooo... eti sasa hivi ni Jenerali hafikiki kirahisi, ama kweli... dunia hii!

Kiwanja chake kiliporwa bila mimi ingekula kwake.

Baada ya kufukuzwa kazi alichanganyikiwa kama Chadema 2020, akaja kuponea kwangu, leo ameota mapembe.

Nguo ya interview aliazima kwangu.

Mimi ndiyo nilikuwa namfadhili bia enzi hizo, sasa hivi aaaa... hana habari na mimi.

Alikuja mjini hata mapishi hajui nikamfundisha ili kusalimisha ndoa yake, sasa hivi anajifanya mjanja wa town.

Mimi ndiyo nimemchangia ela nyingi kwenye harusi yake bila mimi hasingeoa.

Matibabu yake ughaibuni mimi ndiyo nilifanikisha kwa kutafuta michango.

Ule msiba wao mimi ndiyo nilitoa gari, jeneza na chakula.

Mimi ndiyo Mshenga wake lakini siku hizi amenisahau anajifanya mjanja, atarudi siku moja.

Nilisimamia ndoa yake lakini hata simu hanipigii.

Hiyo kazi anayoringia bila mimi angekuwa anasota mitaani.

Ndoa yake ilivunjika mimi ndiyo niliirudisha baada ya Watumishi wa Mungu kushindwa, siku hizi anajifanya mjanja hanijui.

Bila mimi kesi ile ilikuwa inamfunga miaka 30 jela.

Bila mimi hasingeenda Ulaya, hakuwa na ela ya pasipoti, viza na nauli, nimemchangia pa kubwa.

Bila mimi kumlipia deni, nyumba yake ile benki ilikuwa inaipiga mnada.

Bila mimi mjini hapa jamaa angeisharudi kijijini.

Bila mimi TRA, VICOBA, SACCOS walikuwa wanachukuwa mali zake.

Bila mimi hiyo gari yake isingetoka bandarini, siku hizi hata lifti hanipi achilia tu kuniazima gari.

Bila mimi jamaa ange-disco chuo.

Bila mimi hasingebatiza mtoto. Hata Kanisani hajulikani.

Bila mimi Mchungaji hasingeendesha ibada ya marehemu ndugu yake kwa sababu ni mtoro Kanisani.

Bila mimi hasingebariki ndoa, Mchungaji aliishamgomea kwa sababu alishindwa kutimiza vigezo.

Bila mimi jamaa hasingekuwa anapataga safari kazini.

Bila mimi hasingejenga ghorofa hilo analoringia, watu bhana….

Bila mimi Polisi waliishagoma kumuachia.

Bila mimi kumpeleka kwa ndevu-mbili hasingepata mtoto, alikuwa anafuga jogoo asiyewika.

Bila mimi ubunge hasingepata kenge huyo.

Huo uzandiki hapo juu umewakwamisha wengi maishani kwa kuwatengenezea majeraha ya rohoni yasiyopona na majuto.

Epuka makosa hayo kwenye maisha, yatakuchelewesha na yatakuzeesha haraka.
 
Mtoa mada umetoa mifano fikirishi sana..lakn acha nikukumbushe kuwa popote mafanikio yanapoinuka; watu wengi hujitokeza huku kila mmoja akilazimisha uhusika wake utambulike ktk mafanikio hayo wakt si kweli..
 
Mtoa mada umetoa mifano fikirishi sana..lakn acha nikukumbushe kuwa popote mafanikio yanapoinuka; watu wengi hujitokeza huku kila mmoja akilazimisha uhusika wake utambulike ktk mafanikio hayo wakt si kweli..
Ni kweli mkuu,

Mimi nimeamua kuepuka huo mwenendo. Hauna tija.
 
Ni sifa mojawapo ya success..ukifanikiwa kila mtu atalazimisha kukujua toka kabla hujapata..na sio lazima success tu hata famousity..Nonda Papii (DRC) alitokea Burundi kabla hajaja Yanga..Ila alivyong'ara ulaya; Yanga ilijipa sifa maalumu kwamba ndio iliyoibua kipaji chake
 
Ni sifa mojawapo ya success..ukifanikiwa kila mtu atalazimisha kukujua toka kabla hujapata..na sio lazima success tu hata famousity..Nonda Papii (DRC) alitokea Burundi kabla hajaja Yanga..Ila alivyong'ara ulaya; Yanga ilijipa sifa maalumu kwamba ndio iliyoibua kipaji chake
Kinadharia, waliomsaidia Naseeb Abdalla kabla hajawa Diamond ni wengi, wanaweza kujaza uwanja wa Mkapa, binadamu bhana kwa sifaaa...
 
Ukimsaidia mtu ni kama umetoa sadaka kwa Mungu hupaswi kutangaza !

Sema kuna watu huwa wanazingua ndio maana wengine wanashindwa kustahamili wanawapa makavu mubashara!
 
Back
Top Bottom