Epuka Matumizi Holela Ya Dawa

afyakliniki

Senior Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
125
Reaction score
81
EPUKA MATUMIZI HOLELA YA DAWA/MADAWA.

Unaamka asubuhi kichwa kinauma kwa kuwa una haraka ya kuwahi kazini unaamua kunywa dawa za kutuliza maumivu na kuwahi kazini, Mchana wakati unapata chakula unahisi maumivu kama ya asubuhi unamwambia mfanyakazi mwenzio yeye anakujibu kuwa "Ni Malaria hiyo", jioni ukiwa nyumbani unahisitena hali ile ile unamuambia mke/mume wako anakujibu "Si Umeze Dawa za Malaria" nawe bila kipingamizi unameza hizo dawa mpaka zinaisha lakini bado unahisi maumivu ya kichwa yapo.. Wengi wetu tumekua na tabia ya KUMEZA Dawa bila Ushauri wa wataalam wa Afya, Bila Vipimo ili kujua Tatizo/Ugonjwa na wengine Humeza Dawa bila mpangilio.. Hiyo yote tunaita "MATUMIZI HOLELA YA MADAWA"

Mara nyingi dawa zinazomezwa kiholela hutuliza tu dalili za ugonjwa ila sio kuuondoa kabisa, Mfano unapohisi maumivu ya kifua na ukaamua kumeza dawa za kutuliza maumivu itakusaidia kuondoa maumivu (tena kwa kipindi kifupi) lakini tatizo hasa liliopelekea maumivu yale unakua hujalikabili.

Matumizi ya madawa kiholela yana madhara mengi sana kuanzia madhara madogo ndani ya mwili na hata kupelekea kifo, matumizi holela pia hujenga USUGU wa vijidudu vya magonjwa dhidi ya dawa husika.

Hivyo basi wataalam wa tiba na madawa kutoka afyakliniki Wanakushauri wewe Mwanafamilia kutotumia Dawa pasi na Ushauri Wa kitaalam au vipimo toka katika kituo kinacho husika.

Asante na Karibu.
 
Nikweli matumizi holelabya dawa Ni hatari kwa afya na uhai wa mtumiaji,iwe umenunua dukani au umeandikiwa na Daktari yote Ni sawa.
 
Naomba nitoke nje ya mada

Hivi kukaa mda mrefu bila kuumwa kabisa,imekaaje hii??
Kukaa Bila Kuumwa Kwa Muda mrefu ni kiashiria kuwa MFUMO WA KINGA WA MWILI WAKO uko imara.

Hii Sio tatizo na wala usipate Mashaka, endelea kuishi maisha ya kutunza afya.

Asante na Karibu.
 
Ila Kuna Jambo linakera kwa wale madaktari wanao waandikia wagonjwa midawa lukuki halafu mikali mikali bila kujali uwezo wa afya ya huyo mgonjwa kumudu uzito wa midawa hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…