SoC02 Epuka Mazoea kwenye afya

SoC02 Epuka Mazoea kwenye afya

Stories of Change - 2022 Competition

Erny1165

Member
Joined
Jul 31, 2022
Posts
8
Reaction score
5
Hii ni kwa faida ya afya yako na kila anaekuzunguka. Wahenga waliwahi kusema "Mazoea hujenga tabia" nayo tabia hukua kulingana na wakati bila kujali athari zake.

Leo hii naomba niseme nanyi juu ya mazoea ambayo watu wengi tumeweka kwenye suala la zima la afya husysani kwenye matumizi ya madawa.

Ee bwana asikudanganye mtu, utajiri wa kwanza siku zote ni afya na utimamu wa mwili na akili halafu ndiyo hayo mengine yanafuata.

Hii leo wote tutakua mashuhuda kuwa matatizo ya kiafya yameangusha watu wengi sana ambao walionekana kuwa na nguvu kibiashara, kwenye siasa na uongozi, majeshi na hata kwenye sekta za kiimani yaani viongozi wakubwa wa dini za kiimani, hii inatupa picha halisi kuwa haijalishi wewe ni nani au una nini kama huna afya nzuri bado ni sawa na huna kitu kwa maana vyote ulivyo navyo hutoweza vifaidi.

Lakini cha ajabu leo hii watu wanachukulia masuala ya afya kimazoea, ni kwa namna gani iko hivi ambatana nami tutizame.

Hii leo watu wengi wana tumia madawa kwa mazoea hususani antibiotics bila kuzingatia kanuni na maelekezo ya kiafya.

Watu wengi hii leo kuanza dozi na kutoimaliza imekua ni tabia endelevu kwao yaani akinywa siku mbili akajisikia vizuri anaona ndo mwisho bila hata kuwaza ni nini madhara ya kukatisha dozi...

Kama tuu ulikua hufaham au hata kama unafaham naomba nikukumbushe, dozi inatolewa kulingana na kiwako ambacho kinaweza kumaliza vimelea ulivyonavyo inapotokea hujakamilisha dozi basi vile vimelea vinakua havijamalizwa vyote na matokeo yake vitajibadili mifumo ili kuweza kuhimili dawa ya namna hiyo pindi utapotumia tena (resistant mutation) hvyo kufanya hiyo dawa isiwe na msaada tena kwako.

Lakini pia jiulize unapokuaga hujamaliza dozi vile vidonge juwa unavipeleka wapi? Jibu ni unavitupa, kwenye mazingira gani ni wewe ndo unajua ila kumbuka ni kwenye mazingira hayohayo yamkini ndipo vimelea hivi huzalishwa hivyo vina asilimia nyingi ya kuwa na uwezo wa kukinzana na hiyo dawa.

Aidha kumekuwa na desturi ya watu kutumia hizi dawa bila kujua kama kweli anahitaji kutumia na kwa kiasi gani. Hii inapelekea hawa vimelea wanapokuvamia wanakuta hali ya uwepo wa ile dawa ila haina uwezo wa kuwaondoa kwani imeshakuwa hafifu hivyo kuwapa muda vimelea kubadili mifumo na kukinzana na hiyo dawa.

Pia dawa hizi zinaweza sababisha mzio (allergies) kwa mtumiaji kama zitatumiwa kinyume na maelekezo ya wataalam

Sio hilo tuu kuna ile ya mtu kumeza dawa bila kufuata maelekezo, dawa inapoandikwa 2×3 kwa mfano hapo huwa inamaanisha ni vidonge viwili kila baada ya masaa nane lakini kuna watu wanahesabu kuwa ni asubuhi mchana na jion hivyo unakuta mtu anameza kidonge cha kwanza saa 4 asubuhi cha pili saa 6 mchana na cha tatu saa 5 usiku dozi inakuwa haipo kwenye mpangilio mzuri wa muda na kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Lakini pia kuna kundi la watu ambao wameweka mazoea kuwa kila wanapoenda hospitali ni lazima wambiwe wanaumwa na wapewe madawa kitu ambacho si kweli kuna wakati mwili kujisikia vibaya ni mchakato wa mabadiliko kwenye mwili ama pengine ni uchovu ambao hauhitaji madawa lakinj haya yote huwa tunayasahau na kuhisi madakitari hawafai.

Nimewahi kukutana na kisa kimoja cha binti aliyekwenda hospitali akapimwa na kukutwa hana ugonjwa kwenye vipimo akaambiwa aende akapumzike kama hali ikiendelea ndipo arudi hospitali, badala yake alitoka akilalamika kuwa madakitari hawajamhudumia haiwezekani aambiwe haumwi wakati anajisikia vibaya.

Nikagundua hii yote inatokana na mazoea ambayo watu tayari tumejiwekea kuwa tunakwenda hospitali tukitaraji dakitari aseme tunaumwa na turudi na mdawa tele tukameze kitu ambacho sio inavyotakiwa kuwa.

Aidha kuna tabia nyingine ya kimazoea tuliyonayo wengi wetu kuwa hatuendi kufanya vipimo mpaka pale tunapojiona tunaumwa sana kiasi kwamba hatuwezi kufanya chochote hali inayopelekea watu wengi kupoteza maisha kwani unakuta mpaka unakuja kushtuka tayari maradhi yalishakutafuna sana.

Sasa ni nini kifanyike?
Mabadiliko yanatakiwa yaanze kwanza na sisi wenyewe tuondokane na mfumo wa mazoea tulio nao kwenye suala zima la afya kwani afya si kitu cha kutania, mfumo huu tunaoenda nao si mzuri na madhira yake ni amkubwa sana tubadilike.

Lakini pia serikali kupitia wizara na wadau wa afya wajitahidi kuendelea kutoa elimu hii kwa watu kwani kuna wengine wanafanya haya kwa kutojua ni nini hasara za kufanya hayo.

Aidha hata madaktari wanapowahudumia wagonjwa wasidhanie kuwa wote wanaelewa hali halisi jinsi ilivyo hivyo basi wajitahidi kuwa wanatoa elimu ya kutosha kwa kila mgonjwa wanaemhudumia ili anapotoka hapi asiendelee tena kufanya vitu kwa mazoea bali afate taratibu za kitaalamu kwa mfano hilo suala la taratibu za kumeza dawa kulingana na ulivyoandikiwa watu wengi hawaelewi maana halisu ya 2×3 au 1×3 au 3×3 wao wanajua asubuhi mchana na jioni kumbe maana halisi ni kila baada ya masaa nane kuanzia ule mda uliomeza kwa mara ya kwanza.

Pia ifike hatua tufundishane matumizi ya dawa asilia (natural remedies) kama vile mazoezi, mapumziko, maji ya kutosha na dawa za miti ambazo zina madhara kidogo sana kulinganisha na hizi dawa za viwandani.

Kwenye masuala ya afya tuweke mazoea pembeni ili kujilinda sisi na kuwalinda wale tunaowapenda, kwani hii desturi ya mazoea inafanywa hata kwa watoto wadogo ambao bado hawajajitegemea kiakili hivyo madhara tajwa yanawaanza wakiwa wadogo ndio maana unakuta dawa nyingi zinashindwa kufanya kazi kwa huyu mtoto anapofikia umri fulani kutokana na vimelea kuwa resistant kwa hizo dawa...

Tujali afya zetu, tusiishi kwa mazoea
#afya ni mali.

Ni mimi mtumishi wa watu
ERNEST M MPIRA
 
Upvote 1
Back
Top Bottom