Hakuna usawa wa aina hiyo popote duniani. Hata Vatican Papa si sawa na buruda. Usawa unaosemwa ndani ya Katiba ni usawa mbele ya sheria, kupata mahitaji ya msingi, uhuru wa kuabudu na kupata taarifa, n.k. Hata hivyo navyo vinategemea fursa zilizopo na kila mtu anavyozitumia fursa hizo. Serikali inao wajibu kwa kiasi fulani kuhakikisha kuwa haki za msingi zinapatikana lakini yenyewe pekee haiwezi. Lazima mtu binafsi naye ajitume na kupigania haki zake na usawa.