Equatorial Guinea imekuwa nchi ya 24 Afrika kufuta Adhabu ya Kifo

Equatorial Guinea imekuwa nchi ya 24 Afrika kufuta Adhabu ya Kifo

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo aliyekaa Madarakani kwa miaka 43 ametia saini Sheria hiyo mpya itakayoanza kutekelezwa ndani ya siku 90 baada ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali.

Mara ya mwisho adhabu ya kifo kutekelezwa nchini humo ilikuwa mwaka 2014. Pamoja na uamuzi huo, Amnesty International na Umoja wa Mataifa wamekuwa wakiishutumu serikali kutokana na kutoweka kwa raia, kuwekwa kizuizini kiholela na utesaji.

Equatorial Guinea inakuwa nchi ya 24 barani Afrika kufuta adhabu ya kifo baada ya Jamhuri ya Afrika ya Kati iliyofuta adhabu hiyo Mei 2022, Chad mwaka 2020 na Sierra Leone mwaka 2021.

=========================

1663666165324.png

Equatorial Guinea abolished the death penalty, state television announced Monday, citing a new law signed by President Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

The president's son who serves as one of the country's vice-presidents lauded the move he called "historic" on Twitter.

The last official execution in the small country was carried out in 2014, according to Amnesty International. Still, international NGOs and the United Nations regularly accuse the regime of forced disappearances, arbitrary detention and torture.

The measure will come into force in the 90 days following its publication in the official state journal and was approved by parliament in advance.

Equatorial Guinea follows the Central African Republic in May 2022, Chad in 2020 and Sierra Leone last year in recent years' ban on capital punishment on the African continent.

President Obiang, 80, has spent more than 43 years in power, a world record when excluding monarchies.

AFRICAN NEWS
 
Wairudishe tu,Sasa wamekban kwanini?
Kuna watu Ni wanyama Sana Dunia hii kwa hiyo wakikamatwa adhafu ya kifo ndio halali yao.
Hata Pilato alipopelekewa Yesu aliomba beseni lenye maji akanawa akisema mimi dhambi hii hainihusu..

Rais na serikali wamenawa sasa kazi kwa raia km wakitaka kuwamaliza watu km hao kwa adhabu ya kifo kazi kwao

Nawasilisha
 
Madarakani miaka 43, mwanaye ni mmoja wa makamu wa Rais. Mwanawe kasifia hatua hii akiita ni ya kihistoria. Huu ushenzi wa baadhi ya viongozi wa Africa utaisha tu, siku moja. Equitorial Guinea ni nchi iliyo na utajiri mkubwa zaidi Africa kwa ajili ya madini ya mafuta. Lakini wananchi wake wanaishi maisha duni sana. Mwanawe rais ana account marekani Ina takriban dola billioni tano. Serikali ya marekani imezishikilia hizo hela.
 
Death sentence ni ukatili wa kijima, du unaelewa kweli kuhusu mtoto wa president huyu, je hapa kwetu unauelewa huo au ndio u champion wa kwenye I'd fake hizi
 
Dawa ya muuwaji ni kuuliwa tu,
Sasa nyie endeleeni tu kuwalea
Kifo ni adhabu? Nani anawezaa thibitisha hilo? Je marehemu huwa wanaumi?
Jamij inajifunz nn baad ya marehemu kuuwawa?
Huyu anajikosha tu kwa wale jamaa pale ufaransa
 
Kifo ni adhabu? Nani anawezaa thibitisha hilo? Je marehemu huwa wanaumi?
Jamij inajifunz nn baad ya marehemu kuuwawa?
Huyu anajikosha tu kwa wale jamaa pale ufaransa
Ni hivi, anayeua auwawe,
Hakuna lingine,
Vinginevyo ni majuto tu
 
Back
Top Bottom