Eric Shigongo azungumzia jinsi Tanzania ilivyo na rasilimali zenye utajiri

Eric Shigongo azungumzia jinsi Tanzania ilivyo na rasilimali zenye utajiri

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Eric Shigongo, Mbunge wa Jimbo la Buchosa akizungumzia kuhusu masuala ya utalii na utajiri wa Tanzania, amezungumzia kuhusu utajiri mkubwa wa rasilimali zilizopo nchini Tanzania.

Hotuba hiyo ameitoa wakati akiwa katika Kongamano la Kitaifa la Elimu Jumuishi za Kifedha (NFIS) jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuongeza uelewa na ushiriki wa wananchi katika huduma na fursa za kifedha kwa maendeleo jumuishi na endelevu.


Madamu Bi star alikuwepo kikamilifu na kupewa Tuzo ya Mwanachama mwenye miaka 10 katika taasisi.webp
Shigongo akimabidhi Msanii Bi Star Tuzo ya Mwanachama mwenye miaka 10 katika Taasisi ya YEMCO.
 
Swali hili la kijinga wengi huwa wanaliuliza Badala ya kulifanyia kazi na kusonga mbele

Sasa kila kiongozi akiuliza kwa nini sisi masikini unafikiri litabadilika na kuwa tajiri bila vitendo?
 
Yeye mwenyewe kafanya nini Buchosa
 
Ukiwa mtu wa mihemko ni ngumu kumuelewa Shigongo lakini anajitahidi
kuwatetea Watanzania bungeni ili wamiliki uchumi wa nchi yao. Alipambana mpaka sheria ya manunuzi ikabadilishwa na sasa tenda zote za mpaka bilioni 50, hazifanywi na wageni, lengo ni kuwasaidia wazawa.
 
Shigongo amefanya mengi jimboni kwake, Buchosa ya leo siyo ile ya miaka 10 iliyopita labda kama hauijui vizuri. Anapigia sana kelele bungeni kubadilishwa kwa sera ili utajiri wa nchi uwanufaishe wananchi, haina ubishi kwamba Tanzania ni tajiri ila utajiri wake hauwanufaishi wananchi wa kawaida.
 
Ukiwa mtu wa mihemko ni ngumu kumuelewa Shigongo lakini anajitahidi
kuwatetea Watanzania bungeni ili wamiliki uchumi wa nchi yao. Alipambana mpaka sheria ya manunuzi ikabadilishwa na sasa tenda zote za mpaka bilioni 50, hazifanywi na wageni, lengo ni kuwasaidia wazawa.
VERY TRUE MNYONGE MNYONGENI HAKI YAKE MPENI
 
Kama umebahatika kuzunguka nchi hii utakubaliana na Eric Shigongo na kauli hii tuliisikia akiirudia mara kwa mara Hayati Magufuli alale pema peponi.
 
Mimi ni CHADEMA lakini kafika wabunge wanaojitahidi kuwapigania wananchi ni huyu Shigongo, kila video yake hata bungeni lazima aoneshe kuwapigania wananchi..... Japo ni kipindi Kisumu Ila mwamba anapambana aseee
 
Back
Top Bottom