Hemedy Jr Junior
JF-Expert Member
- Feb 17, 2023
- 915
- 1,082
Mcheshi Eric Omondi amekamatwa akiongoza maandamano nje ya majengo ya Bunge jijini Nairobi.
Omondi alikuwa akiongoza kundi la vijana waliojengeka vizuri, watanashati katika maandamano, ambapo waliitaka Serikali kushusha gharama za maisha.
Vijana waliovalia kaptura nyeusi na vifua wazi walikuwa wamesababisha biashara katika maeneo ya bunge kusimama.
Polisi walikuwa wamewaamuru waandamanaji hao kutawanyika, lakini walipuuza kuwalazimisha polisi kutumia vitoa machozi.
Omondi alikamatwa katika ghasia zilizofuata, huku polisi wakimpeleka kusikojulikana.
Vijana hao walikuwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "gharama kubwa ya maisha" gharama kubwa ya umeme" "stima juu, ushuru juu" miongoni mwa machapisho mengine.
Hii si mara ya kwanza kwa mcheshi huyo kuongoza maandamano katika maeneo ya bunge.
Mnamo Februari 2022, Omondi alijifunga kwa minyororo kwenye mchemraba nje ya majengo ya bunge, akiwa na bango kubwa lililoandikwa ‘Cheza asilimia 75’.
Kisha, mcheshi huyo alitafuta usikivu wa bunge kujadili jinsi muziki wa humu nchini utapata angalau asilimia 75 ya uchezaji wa hewani nchini.
Alisema atakuwa kwenye mgomo wa kula na atakaa hapo hadi wabunge wajadili suala hilo.
Imeandaliwa na Kimodomsafi