Erick Omondi awataka mashabiki kutohudhuria tamasha la Alikiba na Harmonize

Erick Omondi awataka mashabiki kutohudhuria tamasha la Alikiba na Harmonize

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
Zikiwa zimebaki siku chache kufanyika kwa tamasha la Afro Vasha nchini Kenya, huku wasanii kutoka Tanzania Alikiba na Harmonize wakiwa kwenye orodha ya wasanii watakotumbuiza siku ya tarehe 11 na 12, mchekeshaji Eric Omondi amewaomba mashabiki kutohudhuria kwakile anachodai kwamba wanamuziki wa Kenya wapewe haki.

"(Hii ina maana kwamba Erick Omondi ni mbaguzi)"

Ninatoa wito kwa kila Mkenya kususia tukio hili. Hawa waandaaji hawana heshima sana. Tulikubali kuwa hatuhudhurii tukio lolote ambalo linadharau kwa nini wasanii wetu wanaonyeshwa katika mabango kwa kuwekewa picha ndogo.

“Ninawapa waandaaji saa 3 kurekebisha tangazo hili la kipumbavu na wasipofanya hivyo nitahakikisha hakuna mtu anayehudhuria tamasha hili. Niamini wewe Afrovasha nakushauri. Badilisha hilo tangazo,”
ameandika Omondi.

Taarifa hiyo aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram umepokelewa tofauti na alivyotegemea kwani maoni ya wengi wanapinga kile alichosema huku wakimtaka aachane na mpango wake huo wakutaka kufanya watu wasihudhurie tamasha hilo.

Kwa upande wao, Kiba na Harmonize bado hawajazungumza chohcote kuhusu kauli hiyo huku baadhi ya Watanzania wakiiomba Serikali ya Tanzania kumpiga marufuku Omondi kuja hapa nchini kufanya shughuli zake za sanaa.

omondi.jpg
 
Erick analazimisha uzalendo uchwara..
Wapambane wafanye badiliko, kuna kipindi kenya eti tulikuwa tunaona wasanii wa kimataifa. Lakini hakuna aliyewasagia hapa walikuwa wanaletwa kufanya show kama wasanii wakimataifa. Ila wasanii walipambana wakageuza meza, hivyo nao badala ya wivu wapambane warudu kwenye zama zao.
 
inakera ila hakupaswa kuja hivi hadharani.
madhara yake ni makubwa kwake kuliko faida aliyokusudia.

sera za kizushi kwenye industry yao ndio zinadidimiza wasanii wao,na hapa ndio huwa nakataa samaki anayesema kenya wana elimu bora kutuzidi,anatumi vigezo gani kuja na hitimisho hili!!!eti haki miliki,hupigi nyimbo mpaka umlipe msanii,kwanini media zisigeulie nje!!!
 
Back
Top Bottom