Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Manchester United imemfuta kazi kocha Erik ten Hag kufuatia mwanzo mbaya wa msimu wa 2024/25. Klabu hiyo, maarufu kama The Red Devils, ipo nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kupoteza mechi nne kati ya tisa za kwanza.
Kipigo cha jana cha bao 2-1 dhidi ya West Ham United, baada ya penalti ya dakika za jioni iliyofungwa na Jarrod Bowen, ambayo ilizua utata, kimechangia kufurushwa. Uongozi wa Manchester United umechukua hatua hiyo kutokana na matokeo haya duni, wakitafuta njia mpya ya kuinua timu msimu huu.
Mkataba wake ulitarajiwa kumalizika Julai 2026, na sasa Ruud van Nistelrooy amepewa nafasi ya muda. Ten Hag alijiunga na timu mwaka 2022 na ameshinda mataji mawili: Carabao Cup 2023 na FA Cup 2024.
Pia, Soma:
+ Mkurugenzi Mtendaji wa Man United: Ten Hag ndiye kocha sahihi kwetu na tunamuunga mkono kikamilifu kwa 100%
+ ERIK TEN HAG kama ataondoka Man United basi itakuwa wameamua kumuondoa tu!