Erling Haaland kutua Man City, mshahara Tsh bilioni 1.5 kwa wiki

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Haaland.jpg
Mchakato wa Manchester City kuelekea kumsajili Erling Haaland wa Borussia Dortmund unaelekea pazuri hiyo ni baada ya kudaiwa kuwa wameshafikia makubaliano ya mshahara wa paundi 500,000 (Tsh bilioni 1.5) kwa wiki.

Man City inataka kukamilisha mapema mchakato huo mapema, ada ya usajili inatwa kuwa ni paundo milioni 63 (Tsh bilioni 190), kama kila kitu kitaensa sawa anaweza kusajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano wiki ijayo.

Hiyo inakuja licha ya kuwa wiki iliyopita Dortmund ilisema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhusu mchezaji huyo ambaye pia anawaniwa na Real Madrid na Paris Saint-Germain.

Source: DailyMail
 
Sasa na hao psg wanamtaka haaland wa Nini Kama sio tamaa tu kuharibia wenzao[emoji848]

Pale mbele Wana Messi,neymar,dimaria,mbape n.k
wana tengeneza galastico yao... madrid haikuacha mchezaji kila aliye bora alinunuliwa... wakajaza mastaa...
 
Du, mshahara wa wiki moja ni bajeti ya klabu kubwa kabisa Afrika kwa mwaka mzima. Vidole haviwezi kulingana.
 
Aliyekutangulia amekutangulia tu mkuu. Daima tutasikia wachezaji wenye uwezo mkubwa wakizitumikia timu za Ulaya tu maana kule ndio wanathamini vipaji vya watu kiuhalisia, wanakupa pesa ili hiyo pesa iwape pesa (Win win Situation)
 
Mchakato wa Manchester City kuelekea kumsajili Erling Haaland wa Borussia Dortmund unaelekea pazuri hiyo ni baada ya kudaiwa kuwa wameshafikia makubaliano ya mshahara wa paundi 500,000 (Tsh bilioni 1.5) kwa wiki.

Man City inataka kukamilisha mapema mchakato huo mapema, ada ya usajili inatwa kuwa ni paundo milioni 63 (Tsh bilioni 190), kama kila kitu kitaensa sawa anaweza kusajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano wiki ijayo.

Hiyo inakuja licha ya kuwa wiki iliyopita Dortmund ilisema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kuhusu mchezaji huyo ambaye pia anawaniwa na Real Madrid na Paris Saint-Germain.
1658127819801.png
 
Back
Top Bottom