Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Ernest Sungura ambaye ni mwenyekiti wa wanaopigania haki ya taarifa, na Mkurugenzu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) amemuomba rais Kuangalia namna ya kubadili sera ya uwekezaji kwa tasnia ya habari.
Aidha ametaja tatizo la kufanya kazi bila mikataba na mishahara kuchelewa kwa waandishi wa habari. Sungura amemuomba mgeni Rasmi ambaye ni Rais Samia kuwa idadi ya wanahabari wengi wanapitia changamoto hizo.
Akizungumza kwenye kongamano la maendeleo ya sekta ya habari nchini amesema kanunu za ajira zinaelekeza mambo mengi kuhusu masuala ya ajira ikiwemo kuwa na mikataba ya kudumu na kama mikataba ni ya muda basi isipungue miezi 12. Ameomba kutiliwa mkazo wa sheria ili kuwasaidia wanahabari kupata haki zao ikiwemo Bima ya Afya, michango ya NSSF na fidia.
Sungura ametaja suala la uhuru wa habari nchini na kuomba vifungu 12 vya sheria ya habari kufanyiwa kazi ili kuipaisha Tanzania kwenye uhuru wa habari duniani.
Kutokana na suala la uchaguzi lililoko mbele yetu, Sungura ametoa wito wanasiasa kupata nafasi sawa kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa wanasiasa ni walaji wakubwa wa vyombo vya habari na huvitumia kwa manufaa yao.
Sungura ameomba vyombo vya umma kama TBC vitoe fursa sawa kwa wanasiasa wote kwa kipindi hiki cha uchaguzi
"Sitaki kuwa mwanasiasa, lakini ninapohitimisha kabisa salamu hizi sitakuwa nimetenda haki nisipolisemea kundi la walaji wa habari wanasiasa, hasa ukizingatia mwaka huu tunafanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani tutakuwa na uchaguzi mkuu. Kundi hili mara zote linataka upendeleo wa wanahabari. Sisi CoRI tunashauri haki sawa kwa wanasiasa wote wa vyama vyote katika kuvitumia vyombo vya habari hususan chombo cha Umma cha Utangazaji kama TBC."