Pre GE2025 Ester Bulaya: Mimi sio CCM ni CHADEMA. Utaratibu wa kutupeleka bungeni ulifuatwa hakuna aliyefoji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Akiwa anahojiwa katika kipindi cha Power Breakfast Clouds Ester Bulaya amesema:

"Mimi ni CHADEMA, (kuhusu kufukuzwa) hayo ni mambo ya ndani ya chama na ndio maana sababu sisi tumesema ni wana CHADEMA tukaenda kutetea uana CHADEMA wetu, na ni njia ya kawaida.

"…Kwanza hakuna mtu yeyote anayeweza kuingia bungeni bila bendera ya chama. Mimi Ester Bulaya siyo chizi nitoke huko nimekurupuka nikaenda kuapa…. Hakuna aliyefoji… utaratibu wa kawaida ulitumika, ofisi ya Katibu Mkuu ikapelewa majina… yaani kama kawaida ambavyo mimi niliapa nikiwa mbunge wa viti maalum nikiwa CCM, nimegombea, majina yanapelekwa tume, nikatangazwa… ofisi ya katibu mkuu ndio yenye ridhaa ya kupeleka majina… Sasa taratibu zote mimi nimeshagombea, nimemaliza, mchakato uko ndani ya chama mimi natakiwa kwenda kuapa. Sasa haiwezekani majina yakajipeleka tume.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"…Ofisi ya Tume ya Uchaguzi ina jina la nani alisaini kwenye ofisi ya Katibu Mkuu, mimi nimefuata mchakato wa kugombea halali kabisa ndani ya chama na majina yakapelekwa kabisa halali ndani ya chama, na ndio mchakato huohuo umefanyika tangu siku ya kwanza ambapo nagombea nikiwa viti maalum vijana CCM, haijawahi kusikika hiyo nani amepeleka majina si ndio? Kwasababu wenye ridhaa wapo. Mimi mamlaka yangu ni kwenye kugombea, majina yameenda kwenye chama nasubiria kuapa. Sasa ukiniambia kuna kufoji naamini ambaye anahisi sahihi yake imegushiwa, yeye ndio anatakiwa aende mahakamani."

Tusishnage COVID 19 wakarudi bungeni kupitia CHADEMA tena! Hii nchi ina maajabu yake mengi sana🤣
 
Niliwahi kushauri kuwa hawa wadada walikuwa wahanga wa siasa za kibabe za Magufuli. Hawakushiriki wao kugushi nyaraka zilizowaingiza kinyemela bungeni bali ni doal ilifanya hivyo, wao walitishwa sana na kupewa viapo vya kutishia uhai wao kama wangekwenda kinyume nana matakwa ya dikteta Magufuli. Walichotakiwa kufanya ni kufanya ungamo na kueleza kila kitu kilichojiri wakati ule kisha waombe msamaha kwa chama chao. Watu wengi walikuwa wanasema wasamehewe lakini kanuni ya kupata msamaha ni kwa mkosaji kukiri kosa na yeye mwenyewe ndiye aombe kusamehewa siyo aliyekosewa atoe msamaha bila mkosaji kukiri kosa lake.
 
Washakunja pesa za kutosha za bunge leo wanakuja na kauli tamu
 
Niliwahi kushauri kuwa hawa wadada walikuwa wahanga wa siasa za kibabe za Magufuli. Hawakushiriki wao kugushi nyaraka zilizowaingiza kinyemela bungeni bali ni doal ilifanya hivyo, wao walitishwa sana na kupewa viapo vya kutishia uhai wao kama wangekwenda kinyume nana matakwa ya dikteta Magufuli. Walichotakiwa kufanya ni kufanya ungamo na kueleza kila kitu kilichojiri wakati ule kisha waombe msamaha kwa chama chao. Watu wengi walikuwa wanasema wasamehewe lakini kanuni ya kupata msamaha ni kwa mkosaji kukiri kosa na yeye mwenyewe ndiye aombe kusamehewa siyo aliyekosewa atoe msamaha bila mkosaji kukiri kosa lake.
Ni sahihi. Warufi wakijenge Chama.
 
Back
Top Bottom