Uchaguzi 2020 Ester Matiko avamiwa na Polisi, Mlinzi wake achukuliwa kama Jambazi, akimbizwa kusikojulikana

Uchaguzi 2020 Ester Matiko avamiwa na Polisi, Mlinzi wake achukuliwa kama Jambazi, akimbizwa kusikojulikana

Katika muendelezo wa ubabe kwa wapinzani, Jeshi la Polisi limevamia ofisi ya mgombea ubunge kupitia Chama cha Chadema Esther Matiko huko mara na kukamata kwa kutumia fujo kubwa.

Matukio haya hivi karibuni yameendelea kutokea nchini ambapo wagombea wa Chadema kila mmoja kwa wakati wake amekuwa akifanyiwa fujo na polisi.

Hali hiyo haikumuacha salama mwenyekiti wa Chadema na hata mgombea urais wa Chadema.

Huu uonevu utakoma lini?
 
Hapa hizi uniform ndio zinatambulisha kuwa hawa ni Askari Polisi ,kitendo na namna ya ukamataji wake hakitofautiani na Makundi ya kihalifu pale wanapo kwenda kumteka Mtu.

Jamaa wame mkamata kibabe sana, Wapinzani tuna dharauliwa sana; sidhani kama wanaweza kufanya hivi kwa upande wa CCM.

Shame Police
 
Na kuna watu bado watampa kura jiwe, kuishi kwenye shithole kazi sana. Hivi kumshika mtu kwa upole mkasema uko chini ya ulinzi kwa sababu hii, twende kituoni, mkaondoka naye kuna tatizo gani?

Mnavamia bila maelezo yoyote mnaanza kumvuta mtu kwa nguvu wengine na silaha, Nyerere aliongelea sana haya na jiwe toka liingie linajifanya smart nchi nzima
 
Nini kilitokea huko nje kabla jamaa hajakimbilia ndani? Kama hakuwa na tatizo nao kwanini katoka nduki kukimbilia ndani,mbona huyo mwingine kasimama kama roboti na hawajamgusa? ,iko shida mahali...
Mkuu CCM imefanikiwa kuongoza na kuwatawala watanzania kwa kuwa 70% ya watanzania ni wajinga Mtaji wa watawala ni elimu mbovu inayozuia mtu kujitambua, kutambua umuhimu wa siasa, uhuru na haki kuwa ndio tunu za taifa lenye maendeleo watanzana huona siasa ni kama ushabiki Simba na Yanga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nini kilitokea huko nje kabla jamaa hajakimbilia ndani? Kama hakuwa na tatizo nao kwanini katoka nduki kukimbilia ndani,mbona huyo mwingine kasimama kama roboti na hawajamgusa? ,iko shida mahali...
Kama hawajamuua utasikia akifunguliwa kesi ya kusambaza picha za ngono mitandaoni , sasa linganisha na nguvu iliyotumika
 
Back
Top Bottom