Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana kupitia chama cha ACT Wazalendo, Ester Thomas amewataka wananchi wasikubali kutumika na wanasiasa kipindi hiki cha uchaguzi na badala yake siku ya uchaguzi wachague viongozi watakaokwenda kuwatumikia.
"Msikubali kuambiwa mmebadilishiwa mgombea ili hali waliomleta mgombea ni walewale, matatizo ya Wananyamagana yatakuwa yaleyale mkiwachagua walewale. Msikubali kutumika chagueni viongozi wa kuwatumikia na sio kuwatumikisha ninyi watu wa Nyamagana," amesema Ester