The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
"Mimi bado ninaongea lugha ileile ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na bado ninaongea lugha ya demokrasia, sasa suala la uanachama au kutokuwa mwanachama ni la maamuzi ya vikao, sasa kwenye jambo hilo, tutaenda kuongea kwenye vikao, kwasababu sisi tulikwenda mahakamani na kudai uanachama ni ishara ya kukipenda chama chako bayana, kwani si kuna vyama vingi, vingine? Mimi ni mwanachama na ninakipenda hiki chama na ninataka uanachama, nikaenda mahakamani, na mahakamani mtu unaenda ukiona haki ipo mahali kwingine? Mahakama ilitoka hukumu kwamba hawa hawakufukuzwa kihalali kwahiyo mahakama ikaamuru baraza kuu liwasikilize tena, bado baraza kuu likiitishwa huko ndipo tutaongea",- Bulaya.
Mbunge wa Viti Maalum Esther Bulaya akizungumza siku ya Jumatatu Februari 24, 2025 kupitia kipindi cha Power Breakfast cha kituo cha habari cha Clouds FM.
Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025