Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ETARO SEKONDARI: MATAYARISHO YA KUANZISHA "HIGH SCHOOL" YENYE SOMO LA SAYANSI YA KOMPYUTA (COMPUTER SCIENCE)
Idadi ya shule ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini:
(i) Shule za Msingi: 120
116 za Serikali na 4 za Binafsi
6 Shule Shikizi mpya zinajengwa
(ii) Shule za Sekondari: 28
26 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi
10 mpya zinajengwa
(iii) High School: 1
Kasoma High School. Haina mkondo wa masomo ya sayansi. Imejengwa Kijijini Kaboni, ikiwa ni sehemu ya Kasoma Sekondari.
Kuongeza idadi ya "High Schools" Jimboni mwetu:
Lengo letu kuu ni kushirikiana na Serikali yetu kuongeza idadi ya "high schools" Jimboni mwetu tukiweka mkazo kwenye uanzishwaji wa "high schools" za masomo ya sayansi
Mwaka huu tumepata usajili wa "high schools" mbili (2):
(i) Suguti High School
Mikondo 3 (PCM, PCB & CBG) ya masomo ya sayansi. Hii ni sehemu ya Suguti Sekondari
(ii) Mugango High School
Mkondo 1 (CBG) wa masomo ya sayansi. Hii ni sehemu ya Mugango Sekondari
Mradi wa ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (fizikia, kemia na bailojia) kwenye sekondari zetu:
Mbunge wa Jimbo anaendelea kuhamasisha na kuchangia ujenzi wa maabara tatu kwa kila Sekondari ya Kata kwa malengo makuu yafuatayo:
(i) kuboresha uelewa na ufaulu kwenye masomo ya sayansi
(ii) kuanzishwa na kuongeza idadi ya "high schools" za masomo ya sayansi
Matayarisho ya Etaro High School:
Kata ya Etaro yenye vijiji vinne (4) inayo sekondari moja iliyoko Kijijini Etaro.
Sekondari ya pili ya Kata hii inajengwa Kisiwani Rukuba na inatarajiwa kufunguliwa mwakani, Januari 2025
(i) Maabara za Etaro Sekondari
+Maabara ya Kemia, ipo inatumika
+Maabara ya Biolojia, ipo inatumika
(ii) Maabara ya Fizikia:
Inakamilishwa na ujenzi wake unachangiwa na Wanavijiji, Mbunge wa Jimbo na Mfuko wa Jimbo.
(iii) Chumba cha Kompyuta:
Kompyuta 25 tayari zimefungwa na wanafunzi wanazitumia.
Kompyuta hizo 25 zimenunuliwa na Northern Illinois University ya USA. Fedha za ufungaji wa miundombinu ya "internet" zimetolewa na Chuo hiki.
Kompyuta hizi na nyingine zitakazonunuliwa zitatumiwa na wanafunzi wa "high school."
(iv) Tenki la Maji: Lita 21,000
Tenki hili linajengwa shuleni hapo kwa ufadhili wa Northern Illnois University ya USA. Ujenzi uko hatua za ukamilishwaji.
Shukrani:
Tunaishukuru sana Serikali yetu kuendelea kutupatia michango mingi ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ya sayansi kwenye shule zetu - ahsante sana!
Vilevile, tunaendelea kushukuru Northern Illinois University ya USA kwa ushirikiano wake wa kuboresha miundombinu ya elimu ya Etaro Sekondari - ahsante sana!
Picha za hapa zinaonesha:
+Wanafunzi wa Etaro Sekondari wakiwa kwenye somo la kompyuta
+Boma la Maabara ya Fizikia likikamilishwa kuezekwa.
KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA SAYANSI KWENYE SHULE ZETU
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Jumatano, 24.7.2024