ETHIOPIA V Kili Stars: Waandishi wa habari za michezo fanyeni utafiti mtutendee haki wateja wenu

ETHIOPIA V Kili Stars: Waandishi wa habari za michezo fanyeni utafiti mtutendee haki wateja wenu

Baba Kiki

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2012
Posts
1,544
Reaction score
943
Inashangaza waandishi wengi wa habari za michezo hapa Tanzania wanaendelea kushangaa ni kwa nini kili stars imepangwa tena na Ethiopia kucheza robo fainali. Baadhi ya waandishi na watangazaji wetu wanakwenda mbali zaidi kutaka kuhusisha hilo na hujuma kwa kuwa eti Ethiopia ni mwenyeji na labda wao wanaona kuna kitu. Wengine wamefikia hatua ya kusema labda ni kwa kuwa michezo hii haina mvuto tena ndio maana wanalazimika kupanga ratiba ovyo ovyo ili eti kuleta angalu mvuto.

Pamoja na matatizo ya CECAFA na ukweli fulani kama kuendelea kupoteza mvuto kwa mashindano haya, lakini waandishi wetu wanapaswa kuwa na uhakika na wanachokisema kwa jamii. Wanashindwa kuelewa kitu kidogo kuwa ratiba kwa maana ya ramani ya mashindano hupangwa kabla, na kwamba baada ya kupanga makundi, waandaaji wa michuano huwa hawana la kufanya zaidi ya kuacha timu zenyewe zijipange kutokana na matokeo ya uwanjani.

Kwa mfano ilishatajwa kuwa atakayeongoza kundi C ndiye atakayecheza na mshindwa bora wa pili (second best loser). N a sas imetokea mshindi wa kwanza wa kundi hilo ni Tanzania na mshindwa bora wa pili ni Ethiopia.

Hakuna hujuma hapo
 
CECAFA taabani........timu zinacheza zenyewe toka kundi moja??
 
ratiba ilisha pangwa hata kabla ya ligi kuanza, tatizo la waandishi wetu ni kama wanalazimishwa vileee maana siku hizi sizioni zile promo...eheee nimekumbuka hivi zile kamati za kuisadidia stars ni kwaajili ya waarabu tu???
 
Hakuna hujuma,watu hawaangalii ratiba!kuna kundi linajiita wachambuz wa soka,hata hawaelewek,wanachafua hali ya hewa
 
Hakuna hujuma,watu hawaangalii ratiba!kuna kundi linajiita wachambuz wa soka,hata hawaelewek,wanachafua hali ya hewa


Tena hawa wachambuzi ndio balaa zaidi, badala ya kuacha takwimu na facts zizungumze zenyewe kwanza, wao wanaanza na ucha-mbuzi wao a.k.a maoni yao tena bila kutumia takwimu
 
Back
Top Bottom