Eti Ali Mayai kakosa wadhamini TFF, inawaaingia akilini aisee

Eti Ali Mayai kakosa wadhamini TFF, inawaaingia akilini aisee

BASIASI

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
9,732
Reaction score
5,006
Nimemsikiliza ndugu yangu Ali mayai nimestuka kusikia Ali aliondolewa kwa kukosa udhamini.

Hizi chaguzi zina vituko kweli yule mdada amefanikiwa wadhamini na Ali akose udhamini inawaingia akilini?

Tunapita tu
 
Tff Ile n taasisi ya takataka
Rushwa imejaa Sana kule ndani
 
Nimemsikiliza ndugu yangu Ali mayai

NIMESHTUKA kusikia Ali aliondolewa

Kwa kukosa udhamini

Hizi chaguzi Zina vituko KWELI yule mdada amefanikiwa wadhamini na Ali akose uduamini INAWAAINGIA AKILINI
TTunapita tu
Td
Wewe ulimdhamini ikandikwa kakosa wadhamini?

Umewahi kusikia mtuhumiwa mahakamni kakosa wadhamini, inakuwaga uongo?

Unajua vigezo vya kumdhamini mgombea urais TFF ama una hara hara tu hapa kama bata?

Unajua wajumbe wake wanatakiwa watoke pande zote za Muungano yaani Tanganyika na Zanzibar?

Unajua huyo mdhamini anapaswa awe na elimu gani na kiasi gani cha fedha kwenye akaunti? na awe anafanua shughuli gani halali ya kumuingizia kipato?

Note: Ingekuwa nyepesi kama unavyodhani basi angeokota wanywa alkasusu pale Karume wamdhamini.
 
Mkuu, ulienda mdhamini ukakataliwa au ume lobby apate wadhamini akakosa au umekalia makalio yako tu
 
Nimemsikiliza ndugu yangu Ali mayai. NIMESHTUKA kusikia Ali aliondolewa Kwa kukosa udhamini. Hizi chaguzi Zina vituko KWELI yule mdada amefanikiwa wadhamini na Ali akose uduamini INAWAAINGIA AKILINI
Sijaelewa unashangaa lipi kati ya haya; Mayay kukosa wadhamini au Mayay kuondolewa kwenye kinyang'anyiro, ila nitakujibu in advance

1. Kupata au kukosa wadhamini ni jambo miongoni mwa muombaji na muombwaji wa udhamini, maana kumdhamini mtu maana yake ni kukubali kuwajibika kwa lolote baya litakalomuhusu. Mfano, mdhamiwa akitoroka na fedha, basi mdhamini utawajibika kusaidia kupata taarifa za mahali alipo. Hata mahakamani kuna watuhumiwa wengi tu tunaona wakikosa udhamini na kurudishwa rumande

2. Kuondolewa kwenye kinyang'anyiro ni jambo la kikanuni. Ukikosa wadhamini walau watano, maana yake haujaaminika vya kutosha, hivyo haustahili kupewa wadhifa mkubwa kama huu. Kulikuwa na nafasi nyingine 19 za udhamini ambazo hazikumdhamini yeyote, hivyo zilikuwa wazi kufuatwa, lakini hata hizo nazo zikakataa kumdhamini Mayay maana hazikuwa na imani naye
 
we ndo bwege kweli unastuka ninin sasa!! kwani wadhamini wanajificha angekuwa amekamilisha taratibu zote form zingeonyesha. tatizo mmezoea mamabo ya kizamani kwamba mtu akipendwa na wana yanga au simba basi haguswi anaingizwa tu kwenye uchaguzi. fuaten taratibu sio kukurupuka. huyo mama alijiandaa muda mrefu ndo maana alikamilisha taratibu zote.
 
Kilichofanyika waliopaswa kudhamini wote walishapewa chao ukienda wakudhamini wanakwambia tayari nishamdhamini mtu
 
TFF ni Muhimili katika Mihimili.muhimu ya Nchi kama.ilivyo kwa Bakwata, Makanisa ya kibinafsi, Simba na Yanga.

Haiwezekan umetoka 'from no where' ukapata nafasi za Taasisi hizo kizembe zembe, na ikitokea umepata kizembe zembe lazima utolewe 'kizembe zembe' kama ilivyotokea kwa Malinzi
 
Nimemsikiliza ndugu yangu Ali mayai

NIMESHTUKA kusikia Ali aliondolewa

Kwa kukosa udhamini

Hizi chaguzi Zina vituko KWELI yule mdada amefanikiwa wadhamini na Ali akose uduamini INAWAAINGIA AKILINI
TTunapita tu
Td
Unashangaa uchaguzi wa TFF, hiyo ni taasisi ndogo tu. Mbona NEC wanafanyaga vimbwanga kuliko hivyo? Hukumbuki alichofanya DED wa Korogwe dhidi ya mgombea wa upinzani kwenye uchauzi mdogo? Hukumbuki alichofanya DED wa Kinondoni Kagulumjuli? DED wa Mlimba unamkumbuka?

TFF ni mfano halisi na hai jinsi tunavyoendesha chaguzi zetu. Tujitafakari.

Vv
 
Wewe ulimdhamini ikandikwa kakosa wadhamini?

Umewahi kusikia mtuhumiwa mahakamni kakosa wadhamini, inakuwaga uongo?

Unajua vigezo vya kumdhamini mgombea urais TFF ama una hara hara tu hapa kama bata?

Unajua wajumbe wake wanatakiwa watoke pande zote za Muungano yaani Tanganyika na Zanzibar?

Unajua huyo mdhamini anapaswa awe na elimu gani na kiasi gani cha fedha kwenye akaunti? na awe anafanua shughuli gani halali ya kumuingizia kipato?

Note: Ingekuwa nyepesi kama unavyodhani basi angeokota wanywa alkasusu pale Karume wamdhamini.
ungetuelimisha siyo unajibu kwa jazba nyingi
 
Unajua wajumbe wake wanatakiwa watoke pande zote za Muungano yaani Tanganyika na Zanzibar?

Ikiwa wajumbe wanatakiwa watoke pande zote za Muungano, kwanini mgombea kutoka pande moja ya muungano hatakiwi?
 
Ikiwa wajumbe wanatakiwa watoke pande zote za Muungano, kwanini mgombea kutoka pande moja ya muungano hatakiwi?
Acha kufikiri kwa kutumia "sehemu za kukalia" , umesikia amekataliwa ama amekosa wadhamini?

Yani hata kama hakidhi vigezo unataka tu achukuliwe kwasababu anatoka upande mmoja wa muungano?
#AchaUpumbavu
 
Kuchambaua mpira sio kuongoza mpira. Hiko Cha kukosa wadhamini pia inaonyesha hawezi kuwa kiongozi mzuri. Atulie aendelee kuchambaua mpira kwenye vyombo vya habari.
 
Nimemsikiliza ndugu yangu Ali mayai nimestuka kusikia Ali aliondolewa kwa kukosa udhamini.

Hizi chaguzi zina vituko kweli yule mdada amefanikiwa wadhamini na Ali akose udhamini inawaingia akilini?

Tunapita tu
Vipi ulimsaidia kutafuta wadhamini?
 
Back
Top Bottom