Eti asijue................How??


Nasikiliza, endelea......!!!
 
Mimi nadhani kuna vitu tunavichanganya katika hizi anga za mapenzi! labda niulize suali, Hivi kumuonesha mtu kuwa unampenda ni lazima udhalilike kwake ndio ajue?

halaf mjukuu mtiifu maneno kama yepi? hebu nipe mifano kidogo.

Hapana si kunyanyasika......kuna baadhi ya vitu ambavyo pale mnapokuwa mmezoeana huwa vinapungua na pale mwenzi wako anapojaribu kuquestion huwa kama vile tunapuuza.......akiifyumu huwa tunaignore na hapo ndo ule usemi wa usimwonyeshe kama umefika saaaana huapply lol.

Mfano hun wako anatamani wenda cinema, na alikwambia muda mrefu tu then siku ya siku unachomoa, akinuna ,,,,,,,,,,,,,,we kwa vile ukionyesha kuhudhunika kwako na kumwomba samahani unajiona kama vile umekwenda an et\xtra mile........na washkaji hawakawii kukwambia unamuendekeza usimwonyeshe kuwa unampenda saaaaaaaaaaana
 
3D kwa leo zingatia hayo nafikiri yanatosha....
By the way kama umepotea fulani hivi....

Yeah, nazingatia sana. Ni kweli nimepotea kidogo. Hata hivyo kuna wakati post zinakuwa sensitive hivyo napoona kuna dalili ntaandika mengi naamua kunyamaza. Mfano ni thread hii.
 
Yeah, nazingatia sana. Ni kweli nimepotea kidogo. Hata hivyo kuna wakati post zinakuwa sensitive hivyo napoona kuna dalili ntaandika mengi naamua kunyamaza. Mfano ni thread hii.



Sema baba usikike... tena mi nafikiri nyie guys tunahitaji zaidi michango for nyie ndo mabingwa wa kukinai...
 

Kumbe unajua kizunguzu? Hongera sana. Mimi siwezi kuishi bila laazizi wangu wa moyo na ubongo tuhaishi ubungo kibagu
 
Hivi....eti nimpende mtu halafu niigize nampenda kidogo ili asiniletee mapozi? Haiwezekani. Nitasema juu ya wasichana:


  1. Si kweli kuwa ukimpenda msichana na ukamwonesha hivyo atakunyanyasa. Ukimwonesha umemfia atakunyanyasa. Nachomaanisha ni kuwa ukimwonesha umempenda kupiliza kiwango cha kutomwonesha dissatisfaction aki-misbehave atakunyanyasa kwa kuwa atakuwa anajua amekosea na huna uwezo wa kuchukua uamuzi wowote. Mvulana au msichana ni lazima amwoneshe mwenza wake kuwa anampenda na pia amwoneshe anaweza kuchukua hatua ya kuachana naye kama atafanya makosa na kuyarudia. Simaanishi umtishe kuwa utamwacha ila kuna namna ya kumwonesha kuwa umempenda na unajitambua katika kumpenda kwako. Namna mojawapo ni kumwambia kuwa unampenda kwa sababu unaamini anastahili kupendwa na kwa sababu unaamini atakuwa mwaminifu na mtiifu kwako. Mwambie, "Honey, kile utachokipata katika uhusiano wetu ni kile nachodhani unastahili na ninachoweza kukifanya juu yako. Kile nachostahili mimi ni kazi yako wewe kunipa. Kama kuna kitu ntachokosea usiache kuniambia nijisahihishe."
  2. Tunachokosea ni kumruhusu mtu awe na wasichana wengine halafu "sisi" tunaishia kulia tu. Unamwambia unamwacha halafu then unarudi, hapo unategemea nini? Usiwahi kumtisha kuwa unamwacha, mwambie kuwa hauridhiki na anachokifanya. Mwambie pia japo hauna ushahidi lakini vitendo na ishara zake zinakunyima amani, mwambie aifanyie kazi hofu yako. Anayekupenda atakusikiliza, asiyekupenda ni kazi kwako kuendelea kumlilia kama moyo wako "umemfia."
  3. Nikimpenda msichana, kwanza ntamwambia, pili yeye mwenyewe ataona tu. Mimi naweza kuandika mashairi....... eti jamani nimpende mtu halafu niogope kumwandikia verse, sasa kipaji changu hiki ntakitumia wapi?
  4. Hata hivyo ni vizuri kuweka kiasi katika mahusiano (Si kumwonesha kidogo unampenda). Kiasi maana yake usinunue kila kitu hata kama uwezo wako ni mdogo, kumbuka wenzi wetu wanajua uwezo wetu. Kama mwanamume una pesa na mwanamke akajua una pesa usimnunulie magari kila siku, atadhani unafanya hivyo kwa kuwa una uwezo, siku nyingine nunua pipi au mdoli. Bei ya mdoli si dalili ya utajiri ni dalili ya kupenda. Sasa kama ataweka nyodo ni juu yake. Ila naye ni lazima akununulie japo leso. Wavulana nawapasha leo: Kama mwanamke anakupenda nakuhakikishia atakuletea hata big g. Ukiona anaomba tu vocha, halipii nauli, halipii msosi, hapigi japo sekunde, anabipu tu, baba... hakupendi. Ndiyo ni mzuri sana. Ndiyo unampenda sana. Ndiyo "unashindwa" kumwacha. ndiyo alikuwa miss Tanzania. Ndiyo anaongea kiingereza. Ndiyo ukimwacha atachukuliwa na Diamond (sorry kwa kumtaja). Ndiyo yeye ni maarufu kuliko wewe. Ukweli ni mmoja tu hakupendi.
  5. MWONESHE UNAMPENDA. AKIRINGA ONGEA NAYE. ASIPOBADILIKA MWAMBIE TENA. ASIPOBADILIKA ACHANA NAYE. USIACHE KUMWONNESHA UNAYEMPENDA KUWA UNAMPENDA. Ila nayempenda naye...........
Anipende mimi kama mimi,
Si kisa eti mi msanii,
Au labda naonejkana sana kwenye Tivii,
Ila wa kunishauri juu ya HIVii,
Si lazima awe na lipsi pana,
Si lazima akicheka awe ana mwanya.

(Ubeti toka wimbo wa Daz Baba ft Mangwea - Wife)
 



Umenikosha mno.... kweli 3D hapa umesikika na i wish hata other guys wawe na the same attitude... Bravo!!
 
Reactions: 3D.
Mapenzi kaz kwel kwel;
kwanza hili suala kwa mtazamo wangu linawakumba walio wengi kutokana na wengine kutumia nafasi hiyo kumtesa mwenzie kwa kufanya kila aina ya vituko akidhania kuwa mwenzie hatakuwa na namna yeyote kwani kwake ndo kafa kaoza,
pili tujiulize kama kweli tutafanya hivo tutakuwa tunamaanisha mapenzi au mateso? Walio wengi wanajaribu kutumia hiyo concept ya kutokuonesha moja kwa moja ili kuyaepuka mazingira ya namna hiyo. Ni mtazamo tu.
 
Reactions: 3D.

Good Good Asha,
Nimeipenda hii.
 

Duh! Wataisoma tu hata ki moyo moyo safi sana 3D.
 
Reactions: 3D.
Unamwambia nimefika tafadhali badili mawazo...muda huo nae anakua kafika kwingine na kafikiwa basi inakula kwako!!!


kwetu USUKUMANI at once tunasemaga DADA NIMEKUDONDOKEA...hapo lazima mtoto wa watu atabasamu tuu bila jibu...
 
Mj1 sante kwa hii topic dear

nway kwa maoni yangu naona hii kitu
iatofautiana na kwa kila mtu kuna wengine wako
very emotion wanapenda kuji express na kuonyesha
upendo wao wote ( I Love you all the time) wana sema hilo
neno na pia kuli timiza..

( situation ya maisha inachangia sana)

kitu kingine ambacho kinachangia sana
ni umri wale ambao wana balehe ndo wanaanza
uhusiano na mwanaume hao wanaweza kuonyesha
na kutoa upendo wao wote ( hawana experience ya kutosha)
na wale waliobobea kwenye relationship/marriage basi na wao
kuna stage zao wengi tulipoanza tulikuwa tunadhani
(this is it) tukaweka 100% lakini kadiri ya muda unavyoenda
ile teenager love inabadilika sio kwamba inaondoka hapana bali
tunai express in different way ... bado tunaionyesha lakini papo hapo
tunahitaji muda wa kupumua...
 

MMMM!! NGOJA NIKAOGE KWANAZA
i wll be back
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…