Eti asijue................How??

Penzi ni kikohozi kulificha huliweziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.................................

Huu wimbo sijui aliimba nani but mie nimecopy and paste @right reserved
 
Penzi ni kikohozi kulificha huliweziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.................................

Huu wimbo sijui aliimba nani but mie nimecopy and paste @right reserved


Fresh Jumbe nadhani.....hahahah
Dena bana kweli kabisa mapenzi hayafichiki ndio maana ninauliza uhalisia wa maneno hayo ya vijiweni??
Ni mara nyingi tunaambiwa na we nae.....ulimwonyesha kuwa unampenda sana ndio maana!! ..........sasa utakizuiaje kikohozi nacho kishafika kooni??!!
 

Ha ha ha huwezi kuficha lakini yako maneno mengi mno watu husema

Eti ooohhh na wewe ulimwonyesha unampenda ndo maana akakutenda hivyo
Ooohhh ukimwonyesha mwanaume unampenda sana atakunyanyasa
Ni maneno yakufikirika sana huwezi kuficha mapenzi kamwe utajaribu kupretend but you will never succeed
 


  1. I knew kuna hazina ya busara imejificha kwa 3D.....ulichokisema hapa ni ukweli mtupu. Penda kishujaa, usipende kidhaifu. Aksante sana mydia wengi tumenyanyasika sana kwa kuishi maisha ya namna hii.......... unajihisi kumpenda mtu mpaka unaogopa kumwambia akikukosea kisa asiudhike akakuacha loh................... ah mi ctaki




  1. Hahahaha hapo ndo pabaya zaidi . Unajua/anakujulisha kuwa yupo mwingine bado wang'ang'ania tu ni mbaya.

    Nikimpenda msichana, kwanza ntamwambia, pili yeye mwenyewe ataona tu. Mimi naweza kuandika mashairi....... eti jamani nimpende mtu halafu niogope kumwandikia verse, sasa kipaji changu hiki ntakitumia wapi?
Hahahahaha nimeipenda hii 3D we kiboko eti bwana raha jipe mwenyewe ati. Wawezatunga nyimbo achia kipaji bana usikifiche...........Aksante leo umenifurahisha sana.



Anipende mimi kama mimi,​


Si kisa eti mi msanii,
Au labda naonejkana sana kwenye Tivii,
Ila wa kunishauri juu ya HIVii,
Si lazima awe na lipsi pana,
Si lazima akicheka awe ana mwanya.​

(Ubeti toka wimbo wa Daz Baba ft Mangwea - Wife)​


Aksante sana 3D. Thats all I can say to this useful post
 
Reactions: 3D.
Penzi ni kikohozi kulificha huliweziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.................................

Huu wimbo sijui aliimba nani but mie nimecopy and paste @right reserved

Aliimba Fresh Jumbe.


Sikinde pia waliimba:

mtu chake apendacho,
hakina hila moyoni,
huridhika kuwa nacho,
japo hakina thamani,
mapenzi hayana kificho,
yaingiapo moyoni,
mwenye mapenzi haoni,
ingawa macho anayo!
 
MwanajamiiOne asante kwa hii topic
Asanteni sana wachangiaji wote mmemwaga point za vungu
Av learnt soo much from you guys

Muhimu kwangu,na hii naahidi kuipractise:
1. Love someone as much as your heart is willing
2. Show your love as much as you can
3. Ingia kwenye relationship na moyo na akili
4. Usionyeshe you are a desperate type
5. You still have a life even if you wont share it with him

Mbarikiwe sana
 

:A S-rose::A S-rose::A S-rose::A S-rose:
 
..... hizi mada nyingine hizi!!:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:
 

Alrite alrite, sasa nimekupata mjukuu mtiifu, hapo sasa hata mimi napinga, penzi sio kuoneshwa tu bali kukolezwa pia ni muhimu, penzi linatawaliwa na hisia na hisia ni lazima ziamshwe kwa vikorombwezo ili penzi liwe active and alive, hauwezi kusema unampenda mwenza wako halafu unaona tabu kumuomba msamaha pale unapokosea au unapofeli kutimiza ahadi.

Na hapa ndipo ninapoona waswahili tunatafsiri mapenzi kwa lugha ya kigeni, ni lazima tujue kwamba kuna vitu ni vya msingi katika mapenzi (eg kutimiza ahadi, outing, kushauriana, zawadi, romantic enviroment, kuwa responsible etc etc), kufanya vitu hivi ni lazima ili penzi lithaminike, lakini waswahili wanatafsiri kufanya vitu hivi ni kuonekana umemilikiwa au kuwezwa kimapenzi au the so called unaonesha mapenzi. big NO.

NINACHOPINGA MIMI.

Mtu kujionesha kuwa yuko very weak katika mahusiano kiasi kwamba mwenza akajua kwamba hata nikileta kidumu/nyumba ndogo ndani basi jamaa atalia tu halaf atanyamaza na hawezi kuniacha. Amini usiamini MJ1, binadamu tukiwekwa juu tunakuwa na kiburi na dharau (hii ni human nature, refer to viongozi wa siasa),
kwahivyo, give love but show strength as well.

THE END
 

Na hii ndio ilitakiwa iwe conclusion ya hii sred. umeipanga vizuri kweli daughter. aiseee! unafanya kazi ya kupanga ratiba za safari za rais nini? lol
imetulia kweli
 
Penzi halifichiki .....ni ngumu kuficha hisia za mapenzi .
 

Mhhhh! MJ1 mie mwenzenu haya ya kuficha mapenzi sijui hata unafanyaje fanyaje ili kumficha mpenzio kwamba unampenda sana! Kama huo wasiwasi wa kutendwa kwa kuwa anajua unampenda sana si bora tu akutende mapema badala ya kuwa nae kwa muda mrefu kisha ukaja kugundua kwamba penzi lake kwako lilikuwa ni usanii tu na si penzi la kweli?

Nimeshaona hapa katika mijadala kama hii wachangiaji wengine walidai wanampenda mpenzi kwa 60% or even less than that! huu si ndio uchakachuaji wa mapenzi!? kama huwezi kumpenda mtu 100% naye akajua hivyo kwanini upoteze muda wako na muda wake kufanya usanii wa mapenzi!?
 
Jamani ukweli ni kuwa if you love someone tell them. Watakuja wengine wataonyesha wanapenda utaachwa kwenye mataa. Hamna haja ya kuficha mapenzi kwani mapenzi ni vitendo sio maneno.
Suala la kuanza kutoonyesha kuwa hujamfia kiasi hicho nadhani ni MATOKEO tu baada ya kuona kuwa hakujali pamoja na kuwa unampenda sana na umemwonyesha hivyo. Yani baada ya kuonyesha upendo wako wote na bado hajali unaweza ukaacha kumwonyesha upendo na ikiwezekana kuachana naye kabisa.
Ila la msingi hapa ni kuwa mtu hawezi jua unampenda kiasi gani mpaka umwonyeshe. Na lazima ajue kuwa akizingua unamtema. Kumpenda kwako sio tiketi yake ya kukudharau na kukunyanyasa.
UKIPENDA ONYESHA, AKIZINGUA ACHANA NAYE FASTA TU.
 
Mimi nashanga sana! hata kuna rafiki yangu mwanaume alimpa ushauri rafiki yangu wa kike eti ajifanye hampendi bwana wake ili jamaa ampapatikie, mie nikipenda nataka ulimwengu mzima ujue including mhusika
 
Na hii ndio ilitakiwa iwe conclusion ya hii sred. umeipanga vizuri kweli daughter. aiseee! unafanya kazi ya kupanga ratiba za safari za rais nini? lol
imetulia kweli

Haaahaha mbavu zangu jamani kuloro,
Ratiba za raisi ntaziwezea wapi mtu mwenyewe alivyo kiguu na njia ivo,
si ntakuwa nawork overtime kila siku.........
 


...so long as hakutakuwa na kudhalilishana i.e "nimemuweka na amejaa kwenye kiganja!," "hapa amefika hafurukuti!"
nadhani ni muhimu na sahihi kuonyeshana mapenzi kwa vitendo!
 

Si kweli. Most likely, hajakupenda from the beginnning.
 
mapenzi ni kikohozi...huwezi kujificha au kujiigiza...litaonekana wazi au la kuzuga huwezi kujificha
 
Nadhani kwa kupretend utakuwa unajitesa sana!

However, love using head more than your heart, keep a a door open, you may need it one day.....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…