Ringo Edmund
JF-Expert Member
- May 10, 2010
- 4,879
- 1,126
Ukimkuta kiongozi anashauri njia ya mkato namna hii ya kumaliza tatizo la mafuta machafu ujue ana matatizo ya akili na ni dalili tosha kwamba yeye pamoja na vyombo husika wameshindwa kazi. Sijui waTZ tunataka ushahidi gani kujua kwamba serikali iliyo madarakani imeshindwa KAZI na inatakiwa ipewe mapumziko ya milele.
Naungana na wote ambao wanawaona hawa EWURA kama watu wasiokuwa na akili timamu kwa kitendo cha kutoa wazo la kuongeza kodi.
Ilikuwa inatakiwa hawa EWURA wote waondolewe madarakani kwani kazi yao ni kupanga bei ya mafuta na kutoa mapendekezo ya kipuuzi huku magari ya watu yakizidi kuharibika na mazingira yakichafuliwa na mchanganyiko wa diseal vs kerosene na petrol.
Kwa upande mwingine hawa TBS nao wanasemaje kuhusu hili maana wanakalia kuvamia madukani mitaani lakini wachachuaji wameachiwa tu wakipata faida kubwa huku magari ya watu yakiharibika.TBS wazee wa viwango ingilieni kati ili kuliokoa taifa.
Na Nyie EWURA mkithubutu kupandisha bei ya mafuta ya taa mjue sisi walala hoi ndio tutaumia zaidi sio wachachuaji.
je hatua gani alichukuliwa baada ya hapo? au mliongea kesho yake
Nadhani usugu wa tatizo hili mpaka kufikia hatua ya magari ya ikulu kuwekewa chakachua ni uthibitisho kwamba EWURA wameshindwa kutimiza majukumu yao. EWURA imepewa jukumu la kusimamia masuala ya umeme na maji.MAMLAKA ya Udhibiti wa Matumizi ya Nishati na Maji (EWURA), imeunga mkono, mapendekezo ya baadhi ya wadau kutaka kupandishwa kodi mafuta ya taa kuwa sawa na ya diseli na petroli. Akizungumza na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Haruna Masebu, alisema endapo kodi hizo zitakuwa sawa na zingine hatua hiyo itakuwa suluhisho kuondoa tatizo la uchachushaji mafuta.
...akataka muongee, ukaondoka...basi end of story. So why telling us all this iwapo unaonekana you did nothing? Pathetic!!...nikamuuliza umenunua lita 4,000 za mafuta ya taa umeyapeleka wapi...hakuwa na jibu akataka tuongee...nikaondoka
Hujamuelewa mkuu, ameongea kifalsafa zaidi. Ni kwamba wananchi ndio wameiweka serikali hii dhalimu ilhali wakijua haiwasaidii, sasa ili waweze kujifunza na kufunguka akili ni lazima haya yatokee wakione cha moto ili wajifunze next time wasichague manyang'au hawa!kwa lugha nyingine unamaanisha uzembe wa ewura kuthibiti hili tatizo ubebwe na mlalahoi ili wao ewura kazi yao iwe ni kukaa tu ofisini na kupandisha bei. hivi umewafikiria watu wanao ishi vijijini kuwa mafuta ya taa ni nishati muhimu kwao, naamini huyo Mungu unaye mzungumzia sio huyu MUNGU wa upendo tunae mjua
sasa ili waweze kujifunza na kufunguka akili ni lazima haya yatokee wakione cha moto ili wajifunze next time wasichague manyang'au hawa!