Eti dawa ya utundu wa mtoto wangu!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Wiki nilimpeleka binti yangu hospitali! Nilipata kitu kipya ambacho nawaomba niwashirikishe!
Binti yangu ana miaka 3.4 Hivi ! Ni mtoto mwongeaji sana na mwepesi wa kukamata chochote anachosikia iwe ni habari ya Tv redia au mazungumzo ya watu,Mf wmaka jana alimwambia polisi tukiwa kwenye dala2 kuwa Mapolisi wanaua waandishi wa habari! akirejea taarifa ya kuuawa kwa Mwangosi!
Lingine kubwa[pengine ndio mzizi wa swali langu ] ni kila manapokwenda ni lazima afanye kitu kam fujo hivi! mfano kanisa atapita mbele kuimba na kwaya nk .
Juzi tukiwa hospitali kama kwaida yake aliniambia anataka kushuka atembee kidogo! nilimwambia atulie si anaumwa ! akasema anataka kuangalia hospitali ilivo.Niliona isiwe tabu kwani ningemzuia angelia basi alipita kuangalia maua na akaenda mpaka ilipo sanamu ya Bikira Maria! na kuichunguza na kuuliza ni kitu gani ! Baadaye akwawa aanamfuta kilamtu mwenye mtoto mdogo ili kumsalimia[walikuwepo watu kam 4 hivi]
Hali hii ilimvutia nesi mmoja mtu mzima !
Akabeba hadi ofisini kwake ! baadaye akaniita .Alichonieleza nilishangaa!
Aliniambia kuwa mwano ni mtundu sana .....kuna dawa inaitwa Vitasquare itamsaidia sana kuondoa utundu na kumfanya awe bright!
Sikuelewa!ALINIAMBIA ZINAPATIKANA PHARMACY!
Naomba kujua hivi hii ni sayansi aina gani!
Je kuna ukweli wowote katika hilo!
Sisi huwa tuna mchukulia kuwa ni kawaida tu na kadri anavyokuwa kuna vingine ataviacha !
Aidha ni kweli anauwezo mkubwa wa kuongea na kujenga hoja kuliko umri wake.....sijahakiksha kuwa na shule atakuwa hivyo kwani bado anacheza Chekekechea!
 
tusubiri waje madakari nawashauri nasaha, ila kama hizo dawa zipo nitamshauri na shangazi angu maana ana mtoto ni mtundu kupitiliza anaongea kila anachokisia hadi maneno machafu mtoto anaongea na hana uoga wa chochote yaan ki ufupi anatia aibu
 
Dah! Isiwe ndo dawa ya kumfanya akazorota kiakili, we ukahisi anakuwa bright
 
Vita square chewable tablets, ni just multivitamin, kama mtoto wako anakula vema sioni haja kumpa madawa yasiyo na maana, other wise kama anaumwa yaani ana vitamin deficiency unaweza mpa ila kama yupo vema sioni kama kunachochote kitachange. Mimi nina mtoto wangu wa 2.5yrs ni mtundu yuko kama wako, ninachokifanya ni kumfundisha vitu vizuri wakati ni mkemea kwa vile visivyofaa. Lakini with time haya yataisha as she grows up. Kikubwa you need to control her behavior.
 
kila mtoto anapokuwa,anakuwa na tabia yake.kuna wengine wakiwa wadogo wanakuwa watundu,ila wakikua wanaacha.wengine wanakuwa wapole wakikua wanakuwa watundu.mfano wengine wanakuwa wanapenda kuangalia cartoon fulani,wakikua wanapenda kitu kingine.ni kawaida tu,muhimu uwe unamuelewesha tu na anapokosea unamrekebisha
 
Pole sana, kwa yote mabaya anayofanya usiache kumkaripia tena kwa nguvu zote, na tena kama mnalala nae chumba kimoja wewe na yeye na baba yake mtakuja kumkataa cku moja atakapowatibulia yote ya ucku. Ova.....! Asante mungu Traves toto langu limetulia
 
Huyo mtoto ni very intelligent! Yote anayofanya ni dalili za akili nyingi na kujiamini.Kama anafanya kitu ambacho ni wazi kipo nje ya maadili, mweleweshe polepole kwa upendo ataelewa sana.Lakini hivi vingine anavyofanya ni ubongo wake tu unachemka. Chekechea aanze hapo nyumbani. tafuta muda umfundishe kuandika na hesabu ndogondgo za msingi.
Utashangaa! I wish I had such a child!
Hiyo ya dawa ya utundu it's just trash!
 
tusubiri waje madakari nawashauri nasaha, ila kama hizo dawa zipo nitamshauri na shangazi angu maana ana mtoto ni mtundu kupitiliza anaongea kila anachokisia hadi maneno machafu mtoto anaongea na hana uoga wa chochote yaan ki ufupi anatia aibu

Umenikumbusha kuna mtoto wa jirani yetu ana miaka mitatu anaelekea wa nne sasa kila akionekana mahali palipo na watu wazima basi lazima wakimbie sababu ya ukorofi wake na maneno machafu anayotoa bila simile.
 
mtaftie vitu vya watoto vitakavyomfanya ajifunze kama vile michezo ya watoto, cartoon zinazoendana na umri wake na zinazofundisha, atakua busy siku nzima lakini hatakua mharibifu -uhakikishe humpi activity moja, awe na nyingi ili zisimchoshe
sioni kama kuna sababu ya kumpa dawa maana mtoto anajifunza huyo......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…