Eti Fimbo ya mbali.... Mke wangu nimruhusu amegwe!

Ngekewa

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2008
Posts
7,705
Reaction score
1,288
Yamenikuta! Naambiwa fimbo yangu iko mbali nikubali yaishe!
Matatizo ya maisha yametufanya mimi na mke wangu tukubali ushauri wa rafiki yangu wa kumruhusu mke wangu akatafute kibaruwa umangani. Rafiki yangu huyo yuko huko kwa kitambo akiwa dereva wa magari makubwa na huja nyumbani kila baada ya miaka miwili.
Anapokuja pesa hujionyesha hivyo alipotushauri tulikubaliana na mama watoto aende akatafute kibaruwa huko kama mtumishi wa nyumbani.
Mama watoto alienda huko akiniwachia ulezi tukitegemea mabadiliko ya maisha. Miezi michache mke wangu akituma pesa kidogo zilizosaidia maisha huku. Mara mambo yalibadilika, mama watoto aliniletea habari kuwa sasa yuko kwenye mateso na hata mshahara wake halipwi. Tatizo ni kuwa mama mwenye nyumba amebaini kuwa baba mwenye nyumba anapiga malaini kwa mke wangu, hivyo kaamuwa kumuonyesha na Baba mwenye nyumba nae baada ya kuvumilia muda mrefu na msimamo wa mke wangu wa kumtolea nje nae kaamuwa atumie mateso na vitisho ili apate mradi wake.
Niliwasiliana na yule rafiki yangu alietushawishi juu ya hali hii nae akashauri mke wangu akimbie kwa mwajiri wake nae atamficha ndani ya gari lake ili kumvusha sehemu alioko ili afike kwenye mji wenye ubalozi wetu. Mke wangu amefanya hivyo na baada ya siku moja tangu atoroke amenitumia ujumbe huu wa simu;

' Tumeshapoteza siku nzima tukiwa njiani na imefika usiku rafiki yako amekodi chumba lakini anachoniambia mimi sikielewi. Ananitaka kimapenzi na nilipomkumbusha kuwa wewe ni rafiki yake alinijibu kuwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka!
Amenikumbusha tu kuwa mimi sina ninapopajuwa na ni mkimbizi. Sijui kama ni kweli lakini amenambia kuwa nikikamatwa na maaskari basi watanifanyia vibaya kwanza kabla ya kunipeleka gerezani. Hadi sasa nimejaribu kukutunzia heshima yako na kwa vile hili la kuja huku tuliliamuwa pamoja naomba ushauri wako lipi la kulifanya?'

Baada ya kuisoma msg hiyo nimechanganhikiwa. Wenzangu nakuombeni ushauri nini cha kufanya katika tatizo hili?
 
Imekaa kimuvimuvi...
 
Ungetafuta ushauri kabla ya kumruhusu kwenda huko ughaibuni maana ni vp alimpeleka yeye? Au endeleza script coz ni nzur
 
Vipi bado yuko kwenye kuvushwa mpaka mida hii
Vumilia ndio ukubwa huo
 
Mimi huwa naswhangaa watu wanawaamini marafiki zao. Wengi wa hawa marafiki huwa wanakuwa si wazuri. Mkuu shtuka
 
Umepost hoja yako majira ya saa 9. Na kama ni arabuni kwa tofauti ya saa 1 ina maana haijawa usiku bado.
Ndio kusema kama hiyo sms ni kweli aliituma usiku ina maanisha sio leo, na kama sio leo basi kuna jambo lishamtokea mkeo!

Kwamba rafikiyo kesha kula au askari wa umangani wamemla, na wale wanakulaga vibaya sana hata kusiko!

Case closed🙂 ushauri wowote hauna maana kwa sasa!
 
uarabuni kuna viza za uyaya?????au mkeo aliendaje???mie nataka nikawe yaya huko lol,nahisi huu wote ni ushigongo....sijui mnapata nini kutunga?ukute wewe na mkeo wote mko hapo mwanakwelekwe...lol
 
uarabuni kuna viza za uyaya?????au mkeo aliendaje???mie nataka nikawe yaya huko lol,nahisi huu wote ni ushigongo....sijui mnapata nini kutunga?ukute wewe na mkeo wote mko hapo mwanakwelekwe...lol

Au Uru Kishumundu (UK)
 
Kitanda hakizai haramu, akirudi na mimba itabidi uwe mpole tu mkuu, sio kosa lake. Ombea mkeo arudi salama tu, there is no way out.
 
Ungetafuta ushauri kabla ya kumruhusu kwenda huko ughaibuni maana ni vp alimpeleka yeye? Au endeleza script coz ni nzur

Zaidi ya kutoka kwa rafiki nimuaminie?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…