Asikudanganye m2 mkuu wangu, yaani ni graduates wachache sana wa SUA ambao wanasota muda mrefu kitaa. Kozi sa SUA ziko very diversified....chukua hata wale wanaosoma purely agricultural courses, huko unakuta units za kutosha za marketing, economics, project management& evaluation,operations research as well as social science researches. Tofauti na vyuo vingine ambavyo huwa wanasoma tu qualitative research; pale wanapiga hadi quantitative na wanaifanyia kazi kwenye special project (disertation) ambapo m2 anatengeneza proposal, anaenda kukusanya data na anafanya hadi data analysis nd interpretation. Kutokana na hiyo diversification, unakuta graduates wake wana-fit sehemu nyingi mno kv serikalini, kwenye research insitution, mabenki na NGOs. Na ndio maana utakuta m2 amesoma kilimo lakini anafanya kazi as loan officer na ana-fit kutokana na hiyo diversification. Na karibu kozi zote wanapiga Biometry....hii ni advanced statistics ambayo kama haupo fit lazima ikumwage mapema kabisa na ni muhimu sana kwenye masuala ya research. Ukiacha kozi hizo ambazo ni purely agricultural courses, kuna kozi zingine kv agroeconomics, environment science as well as wildlife management.....hawa wote ni wachache sana wanasota kitaa kwa muda mrefu. Nakumbuka class ye2, ni wachache sana (tena kama wapo) ambao walimaliza miezi 18 kitaa.