Eti hivi sisi Watanzania wa ovyo ovyo?

Eti hivi sisi Watanzania wa ovyo ovyo?

Tanganyika jeki

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2011
Posts
243
Reaction score
87
Hivi sisi wa ovyo ovyo? Ninatamani ije siku sisi watanzania tuwe na uwezo wa kujitawala vizuri bila kuwa 'ovyo ovyo'.

Ebu fikiri jamii ambayo kwa pamoja itaamua kupambana na uovu unaoiandama jamii bila kuwepo kwa fikra za utambulisho wa aina nyingine kama dini, kabila, mkoa, chama, jinsia n.k.

Ebu fikiri, kinachodhaniwa kutendwa na Prosesa Juma Kapuya ni kiovu. Hakina uadilifu. 'Kutembea' na msichana mwanafunzi wa miaka minne ni kosa kisheria na si sahihi kimaadili. Mamlaka zinazohusika ama zimenyamazia au kupuuza au hazioni hatia. Mfano jeshi la Polisi kupitia kamanda Kova limedai halioni kosa la Kapuya kwani hayo ni mambo yake binafsi. Kwa sababu ni Kapuya hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa. 'Ni mwenzetu'. Labda yule mtoto (wa miaka 14 kipindi kile) ana kiherehere.

Suala zito hili la maadili linageuzwa kuwa ni jambo dogo la fitna za kisiasa! Hata uchunguzi haupewi nafasi kufanyika. Kwenye nchi inayofuata utawala wa sheria na utawala bora hakuna mkubwa wala mdogo wote ni sawa.

Je, ingekuwa vipi kama ni 'mwalimu tu wa sekondari fulani kafanya hivyo? Angeachwa bila kuchunguzwa? Na vipi kama ingekuwa ni kiongozi wa chama cha upinzani? Naye angeachwa?

Jamii ambayo haithamini maendeleo ya watu ni jamii mufilisi. Maendeleo ya watu huhusisha kutimiza mahitaji ya mwili, akili, na roho. Maendeleo ya binadamu si vitu pekee bali ni ubora wa utu.

Mtoto wa miaka 14 ni mtu kamili. Ana mahitaji yake mengi ya msingi kama chakula, maji, elimu, kupendwa, kulindwa nk. Kwa sababu ni mtoto jamii ina jukumu kubwa zaidi la kumlinda na waovu. Ndipo tulipotunga sheria ya mtoto ifanye kazi hiyo. Tukitambua mtoto akili yake haijakomaa kufanya maamuzi peke yake. Mtu mzima hasa wa rika la mzee Kapuya na uwezo na upeo mkubwa wa kiakili. Na uwezo mkubwa wa ulaghai (manipulation). Hivyo, mtoto yule asingeweza kuchomoka kwenye makucha yake.


Ni lazima tujiulize. Jamii ilikuwa wapi kumsaidia mtoto huyo kulipa ada yake bila kulipia mwili wake.


Ni hivi karibuni tumempoteza msomi mahiri wa sheria Dk. Sengondo Mvungi. Ameuawa na wanaodhaniwa ni majambazi. Kwa mujibu wa polisi walienda kuiba pesa na laptop. Watu hao wenye ujasiri wa kukatiza roho za watu wasio na hatia kama Mvungi ni binadamu kama sisi. Walikuwa watoto zamani. Jamii haikuwaongoza vizuri. Miongoni mwao ndio hao wahalifu. Wengine waliobahatika kwenye maisha ni hawa akina 'Kapuya'. Kwa sababu ni hayuko jela, hakabi mtu roba, haui, yeye si mwenye hatia!

Dhana ya uovu kwa jamii ya watanzania ina macho. Inaangalia matabaka, dini, chama cha siasa, jinsia, umri. Uovu unabagua. Kova anatambua hilo. Ndio maana nasema mambo yetu watanzania ni ovyo ovyo!
 
Ebu fikiri, kinachodhaniwa kutendwa na Prosesa Juma Kapuya ni kiovu. Hakina uadilifu. 'Kutembea' na msichana mwanafunzi wa miaka minne ni kosa kisheria na si sahihi kimaadili. !
Are you serious? kama yule binti ndio ana umri huo si profesa angemchana chana.
 
Back
Top Bottom