Eti kosa la kwanza sio kosa awamu ya tano hakuna huo upuuzi

Eti kosa la kwanza sio kosa awamu ya tano hakuna huo upuuzi

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Awamu hii ya uongozi wa taifa hakika itatuletea maendeleo kama taifa. Kale kamsemo ka kiswahili ka kulinda uzembe na ufisadi eti 'kosa la kwanza sio kosa' kameenda likizo au katakua kamekufa.

Kamsemo kanatumikaga vibaya na sisi waswahili eti kila mwizi na fisadi mtumishi wa umma aibe mara moja. Kila mtumishi wa umma wala haibi au kufanya kosa mara moja ila kila akikamatwa utasikia 'asamehewe jamani kosa la kwanza sio kosa'..pambaaf kwelikweli. 😂😂
Heko awamu ya tano wakikukamata mwizi au fisadi wanakulipua hapohapo.

Kufanya kazi ya kuleta maendeleo kwa nchi sio lelemama inahitajika nidhamu na maarifa ya hali ya juu.
 
Ama hilo ndilo lile la kusema Baba wa taifa JPM ni kiboko ya wakorofi huyu tunaenda nae mpaka mpaka afe.
 
Back
Top Bottom