Eti kuna wanaYanga bado wanapoteza mda kumsikiliza Zahera

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Kashindwa amebaki anaweweseka tu. Haelewi afanye nini tena. Amebaki kuwalaumu wachezaji eti hawana malengo.

Muda unaenda siku zinapita na ameshindwa kabisa kuitengeneza timu. Leo Yanga wanamtihani mzito mbele ya waarabu, bila lamli wala unabii au upajo wa maji na mafuta Yanga wanakaa mapemaaaa!

Ndo ukwelii
 
Simba yenye malengo imetolewa raundi ya awali na vibonde UD SONGO, sasa hivi wamebaki kucheza ligi ya mchangani na akina Singida United
 
Malengo ni kusajili Wabrazil waje kucheza na Namungo, Ndanda na Biashara ya Mara. Lengo limefanikiwa Sana.
 
Hakuna mwanamichezo mwenye akili timamu wa kumlaumu Zahera, Uwezo wa Zahera ulijidhihirisha msimu uliopita kwasasa wanaotakiwa kudhihirisha ubora wao ni wachezaji binafsi. Zahera hawezi kuingia uwanjani akacheza mpira, Mchezaji ameajirwa kucheza alafu katikati ya msimu unaongezeka uzito, mchezaji anafundishwa kufunga!! Yaani unasajiliwa alafu ufundishwe kufunga!! Kuwa fit na kiwango bora, kuchezavizuri ni kazi ya mchezaji mwenyewe kocha ni mambo ya ufundi tu. Zahera hana lawama.
 

Niliposoma tu maneno 'lamli' , 'ndo' 'upajo' ni rahisi kufahamu ni mtu wa aina gani...
 
Bongo kuna kaziii
Your browser is not able to display this video.
 
Hii Yanga yetu haiendi kokote! Bora hata tungepangiwa Bandari au Gor Mahia! Ila siyo hii Pyramid. Tujipange tu kwa ajili ya ligi kuu.
 
Hii Yanga yetu haiendi kokote! Bora hata tungepangiwa Bandari au Gor Mahia! Ila siyo hii Pyramid. Tujipange tu kwa ajili ya ligi kuu.
Sawa UD songo.Tumekusikia Na wabrazil pori
 
Yanga hawachezi hiyo ligi unayo iita ya mchangani? Inashika nafasi ya ngapi kama hiyo ligi ni nyepesi kama unavyo iita?
Simba yenye malengo imetolewa raundi ya awali na vibonde UD SONGO, sasa hivi wamebaki kucheza ligi ya mchangani na akina Singida United
 
Nauza yanga mbovu na chuma chakavu... Alisikika mlevi mmoja
 
Hahaaaa.. Mbumbumbu ni mbumbumbu tu
 
Tatizo la baadhi ya mashabiki wenzangu wa Yanga, ni kutokuukubali ukweli. Timu yetu ni ya kawaida sana, hatuna kikosi kipana, usajili wa Zahera una walakini! Kwa aina hii ya timu, HATUWEZI kuwatoa hawa Pyramids! Tukubali tu ukweli.

Kama vipi, tujipange tu kwa msimu ujao! Timu haina washambuliaji! Kocha amemuuza Makambo ili apate 10%, leo hii mbadala wa Makambo yuko wapi? Siku nikisikia Zahera ametupiwa virago pale Jangwani, nitafarijika sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…