Jirani yangu alinikabili na kuniuliza!
Ilibidi nimuulize imekuwaje tena?
"Kuna wakati mke wangu ananipenda nami huwa najuwa hasa kama ananipenda lakini wakati mwengine huwa hanithamini hadi hudiriki kutaka kuachana nae", alinijibu "Hivyo kweli ana mapenzi ya kweli huyu?", aliendelea kuniuliza.
Nimjibu nini na hiyo ni ndowa, nilitamka neno moja tu "Mhn" nikaubana.
Nilibaki na mawanzo na kujiuliza eti kweli hii inawezekana na kama inawezekana nini suluhisho?
Maudhi yanakuja na kuondoka lkn kwa kuwa kuna mapenzi ndio maana wako pamoja!
Mtoto na mama wanaudhiana ingawa mapenzi yapo; binadamu na Muumba wake 'huudhiana' ingawa mapenzi yapo.
Note:
Maudhi yakizidi huathiri mapenzi!
Kuna mambo mengi yanayosababisha ndoa/mahusiano iwe na maudhi lakini haifi.Sidhani kama ni mapenzi,lazima mmoja atakua ana matatizo au wote.Kuna maudhi ambayo ni vigumu sana kuyavumilia,lakini mpaka mtu anapata wazo la kuachana,jua hapo maudhi yapo ya kutosha.Hao hawajitoshi na hawaamini kua bila ndoa kuna maisha.Wanaamini ndoa ndo utu na ndo ukamilifu,ndo maana wanailinda ndoa kwa gharama yoyote ile!
Mtu asikudanganye kama yanakuwa same levele from day one. Labda mwanzoni yatakuwa hivyo lakini later ni mazoea na zaidi saa nyingine inaweza kuwa hata libido hakuna mnaishi kama dada na kaka.
Its cycle, which need to be revive every time it hits you.
Hukiano hivyo hakuna mapenzi hapo!