Eti Masau Bwire Hashabikii Simba Wala Yanga

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Baadhi ya washabiki husema mimi ni Simba, wengine wanadai mimi ni Yanga.

Ndugu zangu wanasoka, sio kila Mtanzania ana mapenzi ya Simba ama Yanga, wapo ambao hawazipendi hata kuzisikia timu hizo, miongoni mwao nikiwa mimi!

Sizipendi timu hizo, sizishabikii, sitazishabikia kwa mapenzi kama wengi wanavyodhani!

Nilizichukia timu hizo ningali mtoto, nasoma darasa la pili!

Ilikuwaje nikaichukia Simba utotoni?

Siku moja nikiwa kijijini Mwiruruma, nikiwa darasa la pili, kaka yangu, ninayemfuata safari ya nne kwa kuzaliwa, Inspector wa Jeshi la Polisi Isaya Bwire, ambaye kwa sasa kikazi yuko Mkuranga, wakati huo akiwa mwanafunzi Nyakato Sec, Kagera huko, wakati wa likizo alikuja na picha za wachezaji wa Simba enzi za akina Sunday Juma, Marotha Thoma, Zamoyoni Mogera, Mtemi Ramadhani na wengineo akaibandika ukutani, chumbani kwake! (Sijui kama yeye anakumbuka).

Mie na utundu wangu kipindi hicho, nilichukuwa msumari mrefu, nikazitoboatoboa picha hizo machoni, zikapoteza mwonekano na ubora wake!

Kaka yangu huyo alinikimbiza umbali mrefu katika viunga vya kijiji hicho, kutoka mtaa wa Mashujaa nyumbani kwetu hadi mtaa wa Namagubo kwa akina Shadrack Sagati wa Habari leo!

Alinishughulikia kikamilifu kaka yangu huyu, alinipiga kiasi nikananilii...kwenye naniliiii......, kisa na mkasa, Simba! Tangu hapo niliichukia Simba, nikawa kila ikicheza naombea ifungwe ili kaka yangu aumie. Alikuwa anaipenda Simba balaa! Ikifungwa hali chakula, mie nikawa nafurahi ikifungwa lakini nilipocheka wakati imefungwa, kichwa changu kilikuwa kinaumizwa na makwenzi kutoka kwa kaka yangu huyo ambaye kwa sasa anasimamia utii wa sheria lakini bado anaipenda Simba!

Katika mazingira hayo, ningeipendaje Simba?

Nilifikiria sana kipindi hicho, ina maana kaka anazipenda zile picha na timu ya Simba kuliko mimi?

Yanga nao ilikuwaje nikaichukia?

Shuleni wakati ninasoma, nikiwa darasa la tano, mwalimu wangu wa Hisabati ambaye namkumbuka kwa jina moja la Kadenge, sijui lilikua jina lake kweli au la utani, lakini alifahamika kwa jina hilo. Labda kama Sagati anakumbuka atanisaidia kwani, tulikuwa darasa moja, huyo alisababisha niichukie Yanga!

Siku moja sikuhudhuria masomo, japo utoro niliuchukia sana kwani nilikuwa miongoni mwa wanafunzi waliokuwa wakifanya vizuri darasani, nimefeli sana katika mtihani nimekuwa wa tatu darasani tena, nilikuwa monitor wa darasa na mtunza wakati (time keeper) wa shule.

Sikuhudhuria masomo siku hiyo kwakuwa siku hiyo tulikuwa na mashindano ya mpira (Chandimu) kati ya Simba na Yanga, mimi nikikipiga katika timu ya Yanga nikiitwa Amasha!

Niliitwa jina hilo kutokana na umahili wangu wa kupiga kona ambazo nilikuwa nikizichonga vilivyo, moja kwa moja hadi golini!

Si mnamjua Ahmed Amasha wa Yanga, mambo yake kwenye kona?

Kama haijaenda nyavuni moja kwa moja, basi Abeid Mziba alikuwa akifanya yake kwa kichwa chake!

Nakumbuka mwamuzi wa mchezo huo alikuwa bwana mmoja aliyeitwa Joram Chiliko. Katika mchezo huo, Simba ilishinda bao 2-1, mie nikiwa nimeifungia Yanga kwa njia ya penalti! Hiyo ilikuwa Ijumaa. Siku ya Jumatatu nikawahi shule, tayari kwa masomo.

Mwalimu Kadende alikuwa anakaa mbali na shule umbali kama wa kutoka Mbezi mwisho hadi feli jirani na Ikulu, alikuwa anatembea kwa miguu, hivyo alikuwa anachelewa!

Alipofika tu, aliniita kwakuwa nilikuwa jembe lake kwenye somo lake la Hisabati, hakuna mwanafunzi darasani aliyekuwa akifurukuta mbele yangu kwenye somo la Hisabati!

Alinihoji kwa nini Ijumaa sikufika shule, nilimweleza ukweli kwamba tulikuwa na mechi kati ya Simba na Yanga nami nilikuwa tegemeo kwa timu ya Yanga!

Nilishikishwa masikio, miguu ikaishiwa nguvu, nikatetemeka mwili mzima, nikatandikwa fimbo zaidi ya 20 kisha nikapewa adhabu ya kuchimba shimo la choo, adhabu iliyoniweka nje ya darasa kwa wiki nzima, kisa Yanga!

Baada ya adhabu hiyo, mwalimu Kadenge alinipiga mkwara akidai hasisikie tena habari ya Yanga, akisikia atanitoa macho!

Nani anapenda apofuke kwa ajili ya Yanga! Japo nilibaini mwalimu Kadenge alikuwa Simba, tangu hapo niliachana na Yanga, na kuiona kama adui yangu!

Mimi kama mtu wa mpira, pamoja na kutokuwa na mapenzi ya Simba na Yanga, timu hizo zinapofanya vizuri sinabudi kuzipongeza!

Mimi sishabikii wala sitashabikia Simba na Yanga nieleweni hivyo, huo ndio msimamo wangu. Zikifanya vizuri nitazipongeza kwakuwa mimi ni mtu wa mpira, mpira siyo uadui ni upendo, amani na mshikamano!

Simba umoja daima.....

Yanga daima mbele....

Ahsanteni!

 
Bwire we ni Yanga tu kutokana na maelezo yako hahaha karibu kundini Daima mbele nyuma mikia penda ww
 
Kama ulishawahi kutoa jasho lako kwa ajili ya kuilindia heshima timu pendwa ya yanga kwann sasa uikane hadharani!!!
Masau Bwire wewe ni yanga damu bwana.
 
Bwire atakuwa Yanga ukisoma between the lines. Kwanza alitoboa picha za wachezaji wa Simba, pili alikuwa akiichezea 'yanga' ya huko kwao, tatu alikuwa anatamani simba ifungwe ili kaka yake aumie, so aseme tu yeye ni yeboyebo
 
Stori hii inatufundisha kwamba masao bwire ni yanga damdam
 
Stori hii inatufundisha kwamba masao bwire ni yanga damdam
Na inatufundisha kuwa masau Bwire haipendi simba na anaichukua sana mpaka akafikia hatua ya picha za wachezaji wa simba kuwatoboa macho.
 
huyu masau bwire ndo nani wakuu? naona mi simjui kabisaaa
 
hawezi kusema yeye ni YANGA kwa sasa labda kama ameuchoka ugali wa ruvu shooting
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…