Eti Mhadhiri anatoka Dar anakuja kufundisha Dodoma ina maana kuna uhaba sana wa vijana kuziba hizo nafasi?

Eti Mhadhiri anatoka Dar anakuja kufundisha Dodoma ina maana kuna uhaba sana wa vijana kuziba hizo nafasi?

Ego is the Enemy

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
8,201
Reaction score
16,246
Habari zenu wana jukwaa!

Nimekuwa nikijiuliza sana hilo swali mpaka sipati jibu. Eti lecturer anatoka Dar Anakuja kufundisha Dodoma INA mana kuna uhaba sana Wa vijana Wa Ku cover hizo nafasi.

Kuna vijana wanaingia vyuoni kwa alama nzuri sana na ambazo sio za kubahatisha kabisa na wana uwezo mkubwa sana tena sana ila cha ajabu Mtu anatoka na lower second.

Afu Hao wazee why don't encourage GPA kubwa wanakuambia kuwa wao wanataka MTU practical awe fiti ama unataka uwe academician.

Pia kuna watu wanasoma hapo hata masters yaani hawatoboi wengine wanaishia njiani ila akienda nje anarudi na masters yake fasta.
MIE nachoona kuna ile wewe kuteseka kutusua so unataka kila mmoja apitie njia zako.

Mpaka unaapa kuwa mwanangu inabidi ahaso kama mie. Sasa kuna mana gani ya wewe kuhaso. Inakuwa je MTU anatoka nje k.v ni prof alikuwa anafundisha huko ila akija hapa tz anataka athibitishwe na jopo LA Profesa Wa tz, na hii ishu kumbuka kuwa ni kwa wabongo tu.

Sasa sijui hata Profesa mzungu akija wanamkatalia kuwa wewe sio prof mpaka tukupitishe huku kwetu tukuhakikishe. Najiulizaga sana maswali ila nashindwa kupata majibu. Naombeni mnisaidie kama kuna wazee Wa idara huku mnijibu.

Kuna Dkt mmoja sema akiwa hana Phd akiwa na masterz alimfundishaga mtu akambania sana ila akatusua bana. Akaenda nje anakapiga masters yake mpaka PhD akarudi aliyemfundisha bado ana masters yake. Ikabidi na huyu ticha wake Wa undergraduate akasome PhD nje sasa kibembe kilikuja kuwa anayetakiwa akusimamie ni Fulani yule yule denti wako uliyembaniaga akiwa undergraduate. Bana nakuambia huyu jamaa ilibidi akaichukulie PhD yake huko mahakamani mana alimbaniaga ile mbaya.

Ni kwa nini chuki zisiwekwe pembeni mfano umekosana tu na jamaa anakufundisha ila anakukamata kimakusudi ama umegongana naye kwa demu. MIE najiuliza haya personal conflict yanahusiana vipi na MTU ameulizwa swali akajibu vizuri Je ni kwa nini asipewe alama zake ila mpaka zile chuki zinahamishwa kumpatia MTU alama ndogo ama kumkosesha kwa chuki tu ili kama kumkomoa Fulani.

Pia mfano hili just hearsay Dr akampenda binti akaomba mzigo akakataliwa ila anambania tu ili asifaulu alibebe somo lake kama kumkomoa kwani mapenzi ni lazima ama MTU kuwa na hadhi Fulani BASI anajihakikishia kila kitu atakipata maishani mwake?

Unakuta MTU yaani alisoma sana kwa kukesha sana yaani kwa kuumia sana ile mbaya anataka kila mmoja ahenyeke ndo amsogelee na sio kupata alama kuzidi yeye hapana.

Kuna mizee eti inaapa MIE angali nipo hapa hakuna atakaye first class GPa mpaka nife. Sasa haya ni maisha. Mwanafunzi kama Anakuja na Gari Kali kuliko wahadhiri wake wanaleta chuki usikute wakataka kumkamata kimakusudi. Lecturer anajisifia kukamata watu sapu eti kosta tano wamejaa niliowakamata.

Ama ni ile ile roho ya kiafrika na kimasikini na ya ngozi nyeusi.

Kama kuna sehemu nimeteleza kumbuka namie nitakufa sintoishi milele
 
Hii Tabia ni ya kitoto naweza sema binafsi.

Kufanikiwa kwa mtu mwingine hakuzuii kufanikiwa kwako

Usijaribu kukanyaga watu ili wewe ufike juu wakati watu wanaumia huu ni Ujinga

Ila kiukweli ni kutokuwa na utu ndio chanzo kikubwa sana hapo
 
Bure kabisa...eti huyu naye yuko chuo??!!
Kazi ipo kwa kweli..
 
Gpa kubwa pekee haikufanyi uwe lecturer mzuri. Ndio maana kuna interview... Na sio wote wanye gpa kubwa wanapenda kua malecturer.

Pia kuna kozi nyingine zina uhaba wa wataalam ni sawa na ilivyo kuwa huko chini, walimu wazuri wa hesabu na physics walivyo kuwa wachache.

College yetu nakumbuka tulikuwa tunafundishwa na wahindi hadi warusi kutoka india na russia.
 
Hujui kuwa kuna malecturer wanatokaga hapa wanaenda kufundisha South Africa na wakati huo huo ni malecturer wa vyuo vya hapa hapa nchini.
 
Jaribu Ku samarize uweke in presentable way and easy kusomeka kwa wengine. Mana sio wote wenye uwezo Wa kusoma kitabu.
Pia hii MIE niligundua tu nilipokuwa chuoni
Una hoja za msingi ila uandishi wako sasa.

Shida ni kwamba walimu wa vyuo vikuu wamepewa mamlaka makubwa sana hvyo wanaamua kutumia vibaya vyeo vyao.
 
Gpa kubwa pekee haikufanyi uwe lecturer mzuri. Ndio maana kuna interview... Na sio wote wanye gpa kubwa wanapenda kua malecturer.

Pia kuna kozi nyingine zina uhaba wa wataalam ni sawa na ilivyo kuwa huko chini, walimu wazuri wa hesabu na physics walivyo kuwa wachache.

College yetu nakumbuka tulikuwa tunafundishwa na wahindi hadi warusi kutoka india na russia.
Ila kuna limit ya GPA bana. First class ni more preferable ama nakosea
 
Ndicho nachoomaanisha kuwa ni lazima ujikombe jikombe kwao.
Katika taasisi ambazo zina kujuana kwingi ni hivi vyuo vikuu. Hata uwe unajua kiasi gani na GPA kubwa kama wakiamua kukubania utabaki kua mtazamaji tu.
 
Kuna jamaa mmoja aliachwa kuchukuliwa akachukuliwa Wa chini yake kisa tu ya chuki za MTU mmoja ivi anajiona kuwa anafaa sana kuwa pilato.
Una hoja za msingi ila uandishi wako sasa.

Shida ni kwamba walimu wa vyuo vikuu wamepewa mamlaka makubwa sana hvyo wanaamua kutumia vibaya vyeo vyao.
 
nikikumbuka SUA nahisi kutapika, walishaniharibia future yangu ya kuwa prominent academician. Kikubwa ni zaidi ya roho mbaya
Pole mkuu..
Kuna watu hapa badala ya kuangalia mantiki ama logic wao wamejikita kukosoa uandishi MIE sio mwandishi.
Mfano kama nimesoma maths tu huo uandishi Wa kupangilia content nitautoa wapi. Pia kuna mgawanyiko Wa kazi na vipawa mpaka MTU anavuka 25yrs hajajua Bado tuna safari ndefu.
 
Back
Top Bottom