Ndio bibie unaweza kuoka mkate, keki, nk kwenye microwave oven. Mkate utaiva vizuri sana ila kwa kuwa joto la microwave linaenea kwa usawa ndani na nje mkate utaiva ukiwa mweupe wote ndani na nje. Kisaikolojia tumezoea mkate uliobadilika kuwa brown kwa nje mradi haujaungulia. Mkate mweupe kabisa hautavutia mlaji japokuwa umeiva. Ili kutatua tatizo hili unaweza kuuzungushia foil paper. Foil huwa inapata joto sana na kubadilisha rangi ya nje ya mkate, keki, n.k ili mlaji ale kwa amani.