Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,762
- 59,204
tena kubwa sana
- Mgaya na wanachama wote wa TUCTA
- Vyama mbadala vyote vya kisisiasa
- Makonda ,Wapiga debe ,madereva
- Na hata wale madada wauza "utamu"
- NGO
- I mean wananchi wote
Chenge akiwa Spika tunaomba wenye uwezo waorganise migomo na maandamano. Tunapoeleka People's power inahitajika. Wabunge wa upinzani sauti yao bado ni ndogo.
Chenge hajashiinda uspika lakini kitendo cha yeye kugombea ubunge na sasa kuchukua fomu ya spika ni tusi kwa watanganyika
Wananchi wa Bariadi hawana makosa usiwalaumu, walaumu NEC waliolazimisha kurudi kwake pamoja na mafisadi wengine.Yani huyu mzee wa vijisent hafai hata kidogo. Inamaana yeye anaenda bungeni kutetea tena ufisadi? Nilifikiri atakuwa amejifunza kumbe hakuna kitu kabisa. Sijui kwa nini wanachi wa barihadi wamemrudisha tena huyu jamaa
Yaani hii nchi ukiwa na fwedha basi wewe una uhakika....Yaani kwa kesi alizonazo Chenge ningekua nazo mie ningekuwa naiwaza KEKO/ Ukonga au SEGEDANSE (SEGEREA). lakini haki ya mungu huyu Chenge Msengenyaji wala hawazi kuwa kuna jela... ndo kwanza anawaza uspika koz ana uhakika wa kushinda kesi zake za mauaji......Anajiamini nini huyu Jamaa??? nani anamlinda mpk anatuona sie mafala kiasi hiki???
Tena anasema "kiongozi aliye tayari kujitafutia na kujitwalia umaarufu au ushujaa wake binafsi kwa njia ya kuwahujumu, kuwaumiza na kuwachafua wengine kwa kutengeneza tuhuma na kashfa za kila aina" Ila cha kushangaza huyu Msengenyaji hakanushi wala kukubali kuwa hizo tuhuma zilizojadiliwa katika Bunge lililopita ni za kweli au au uongo.... Kwa nini hao waandishi walikimbilia kumtafuta 6 na hawakumuuliza hilo swali??? tena 6 aliwatoa sana koz pamoja na kujadiliwa kwa kashfa hizo lakini zilikua zikiisha kibingwa kwa mtindo wa siku zote wa kubebana.....koz kasema hatagombea tena am sure safari hii 6 akiupata uspika atakua anakamua mwanzo mwisho......
CHENGE UNAJISAFISHA KUONEKANA MSAFI ILA UKWELI HATA WEWE UNAUJUA KUWA WEWE SI SWAFI NA SALAMA.........Kawazuge watu wa SAPIWI.....sio watazania wote....