Rafiki yangu pole sana unachosema kina logic kubwa ila sijui uelewa wako upoje juu ya masuala ya ndoa,maana hata mimi nilipitia changamoto hizo 2008/2009 nilipotaka kuoa mchaga na nimeoa na anakubalika na kupendwa nyumbani sana na ni msaada mkubwa sana kwangu maana wanaujua ujasiriamali haswa.Tatizo ni uelewa wako binafsi je unajua maana ya mke?au urembo wa mwanamke?wewe kumpenda sio hoja ya msingi wala yeye kukupenda sio jambo la msingi,maana kumpenda mtu ni natural ila hoja ni je ANAFAA KUWA MKE,kama wewe ni mchaMungu na yeye akawa hivyo tena sio kinafiki bali kwa vitendo its ok.ila kama ni za kichuochuo basi umepotea.Pia ni ngumu mtu ambaye tayari umeshaanzisha nae mahusiano ya kimapenzi eti ukajua uzuri au ubaya wake,Kama unajua vigezo vya mke mwema na unaamini anavyo sidhani kama ungeogopa wazazi ila kama unabahatisha umepotea.Fanya research utagundua hakuna kabila lenye wake wazuri,mara uchawi,limbwata,uvivu,kujaza ndugu zake,kula sana,uchoyo,ugomvi,uhuni,kupenda shughuli,kutojali ndugu zako,matumizi mabaya ya fedha,kila kabila lina kasoro.Cha msingi ni sifa binafsi za msichana na ni lazima ajue mapungufu ya kabila lake na kwanini yeye sio kama wengine.Kama anafaa anaonekana hata kwa macho tuu(kwa sisi wanasaikologia)angalia nidham yake ya fedha kwa sasa utamjua tuu.Waheshimu wazazi lakini pia unaweza kuwashauri kwa upendo kama unauhakika na msichana.Ndugu zangu wengi na marafiki walionishauri nisioe mchaga nilikaa miaka mitano bila kuoa lakini wao waliooa makabila yao na mengine waliyodhani ni bora ndoa zao ni shida tupu ni mateso mie naishi maisha ya amani na upendo na wengi wananionea wivu maana ndoa yetu ni ya mfano.Muda mfupi tuu tangu tufunge ndo tulombwa kusimamia ndoa nyingi mno mpaka leo ni kielelezo bora.UKIMUOMBA MUNGU MKE AU MME MWEMA NA BORA NA MWAMINIFU USIMPANGIE KABILA YEYE WOTE NI WATU WAKE ANAJUA NANI NI MWEMA NANI NI MBAYA HATA KAMA ANAISHI KANISANI AU MSIKITINI,MIMI YOTE YALINIKUTA KILA NILIYEPATA ALIKUWA HAFAI MPAKA NIKATUA KULEKULE,JIWE WALILOKATAA WAASHI SASA NDIO JIWE KUU LA PEMBENI.MWOMBE MUNGU AKUSAIDIE......KAMA WEWE NI MUME MWEMA UTAPATA MKE MWEMA LAKINI KAMA SIO..FORGET IT HATA UCHAGUE MAKABILA YOTE UTAOA MBAYA TUUU..MAANA IMEANDIKWA NITAKUPA MSAIDIZI WA KUFANANA NAWE NA SI VINGINEVYO.GOODLUCKY.