Eti tukitumia rangi tofauti na nyeupe au nyeusi tunakaziaje?

Eti tukitumia rangi tofauti na nyeupe au nyeusi tunakaziaje?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waswahili tuna kawaida ya kukazia maneno, hasa kwenye rangi kama ikiwa rangi moja

Mfano

Nyeupe... Pee!!
Nyeusi... Tii!!

Sasa je rangi kama
Nyekundu????
Njano???
Blue nk.

Tunakaziaje?
 
Ngoja niwahi hii ya dirishani maana hapa watakuja wazee wa nomino na vitenzi viisishi
 
Waswahili tuna kawaida ya kukazia maneno, hasa kwenye rangi kama ikiwa rangi moja

Mfano

Nyeupe... Pee!!
Nyeusi... Tii!!

Sasa je rangi kama
Nyekundu????
Njano???
Blue nk.

Tunakaziaje?
Zingine hazina kivumishi cha kukazia kwa vile sio rangi za msingi kama hizo mbili ambazo ndio chimbuko la rangi zote
 
Unaendeleza tu,
Nyeupe pee
Nyeusi tii
Nyekundu nduu
Blue uu
Njano oo
Kijanii ii

Yaani hizo irabu za mwisho unaongeza mbili, kasoro kwenye nyeusi tu ndo tunaweka tii badala ya ii ili isifanane na kijani.

Akili za mning'inio hizi.
 
Hizo zilizobaki ni kuongeza tu mkazo kumaanisha ukolevu wa hizo rangi
Nyekunduuu
Njanooo
Bluuu
 
Umeshawahi kuongea hivyo na ukaeleweka. Mfano. Tunaposema uchumi wa kibuluu tunamaanisha buluu uuu
 
Hizo zilizobaki ni kuongeza tu mkazo kumaanisha ukolevu wa hizo rangi
Nyekunduuu
Njanooo
Bluuu
au tuweke tu maneno mengi like

"Ile rangi ilikuwa ya njano, unajua njano, ile ilikuwa njano kwelikweli"
 
Sure maana lenfo si ni kuvumisha tu ama nn

Nyekundu = nakwambia ilikuwa nyekundu kama damuu
Kijani = Kijani kibichii, au nzito hivi kama ya jeshi
au tuweke tu maneno mengi like

"Ile rangi ilikuwa ya njano, unajua njano, ile ilikuwa njano kwelikweli"
 
Back
Top Bottom