Eti uzee dawa!!!

Eti uzee dawa!!!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,768
Reaction score
2,361
Jamaa aliingia porini kuwinda na mbwa wake mzee licha ya kuchekwa sana na wenzake.
Ile kuingia porini tu, fisi huyo akajitokeza.Yule mbwa kwa uzoefu akakusanya mifupa na kuimung'unya mun'gunya huku akitamba kuwa kafisi haka kalikuwa katamu sana.
Fisi kusikia hivyo akaulaza,maana kusikia mbwa kala fisi sasa yeye hakutaka kuwa mfano.
Kwa mbali sana tumbili aliona yote haya na kumkimbilia yule fisi, na akampa stori yote kuwa kadanganywa.
Hao wakarudi wote fisi na tumbili ili sasa lieleweke na fisi apate mlo wake.
Kwa mbali mbwa mzee alipowaona akaitikie, "ehee chakula hiko,tumbili wangu umemleta yule fisi aliye kimbia?"
Kusikia hivyo fisi akaulaza mara ya pili na asirudi tena
Jamaa na mbwa wake wakawinda na kurudi salama
Eti uzee dawa!!!
 
Ujanani ukiishi maisha ya kumpendeza Mungu Busara zitaonekana uzeeni!
 
Mara nyingi na kwa uzoefu, wazee asilimia kubwa huwa na busara ya kutosha. Ni wazi kuna exceptional cases za wazee ambao wana'misbehave".
Busara si kuwa na mvi!...Ni mchanganyiko wa uelewa, mifano na kuona matukio mengi sana yanayoendana na suala lililo mbele yake, na hivyo inakuwa rahisi kwake kutoa suluhu iliyo bora...ndiyo busara hiyo!..Kwahiyo, kwa asilimia kubwa, uzee ni dawa!
 
hako ni kauzoefu sio uzoefu... haha haaa nimecheka sana
 
Exposure na kukubali mabadiliko ndicho kiwapacho wazee busara
 
Back
Top Bottom