Mcheza Karate
JF-Expert Member
- Jun 30, 2011
- 690
- 350
Eti wana JF wapi naweza kuuza asali ya nyuki wakubwa kwa jumla kwa DAR ES SALAAM?
Na je naweza kuuza kwa bei gani?
Natanguliza shukrani zangu kwa wale watakaonisaidia
Kama hutajali nenda Honey King pale Kibaha kiwandani ili ujue bei zikoje kabla hujaingia mikononi mwa Wajanja. Simu yao sina ila kiwanda kipo barabarani kabisa upande wa kushoto kabla hujafika Mlandizi.
utakapokuwa tayari mi nahitaji ya jumla mkuu.
Malila acha udalali.
Ujue jf ni kama ubao wa matangazo kiasi kwamba habari ikifika hapa haiwi yako tena, inakuwa ya jamii yote, sasa wenye asali majumbani wako wengi sana, tatizo soko zuri wanakosa. Muuliza swali huyu anawakilisha kundi kubwa, majibu tunayompa lazima yawe yanajitosheleza ili hata wasiojitokeza wafaidi, mimi nikiwa mmoja wapo, tayari nina mizinga mitano porini. May 2013 natarajia kuanza kupata mavuno ya kwanza, kwa hiyo utaona maoni yangu pia yanawabeba na wengine wanaofuga nyuki.
Kwa hiyo wewe mwaga vitu hapa tuanze kukuletea asali mbichi toka shamba.
Malila sema wewe mkulima/mrinaji wa asali bei yako ili nijue pa kukamatia.