Mito, mie mnaniudhi. Mnafuata wanawake vimeo, wasio size zenu afu unarudi kulalama hapa! Akhuu! Unataka mwanamke mwenye maadili, shurti uwe na maadili kwanza ww ndo umpate!
Kwani ukifolenishwa una wasiwasi gani wakati wewe ndo unakuwa mwanzo wa mstari? Mtaipata mwaka huu wallah!
Ahaa mkuu naona sasa una mpango wa kunichonganisha na wadada wa JF
hayo ni mawazo ya wanaume wasiojiamini!
Kaukweli kwa mbaaaaaali..........ila si unajua in every law kuna exception?!?!?!
just jiamini na uingie kwenye ndoa, think positovely with no assumptions! UKISEMA LIWALO NA LIWE NDIO HIVYO MWISHO WAKE UTAANZA KUONA U-DHAIFU!!!
Acha uongo wewe!!Je,law of floatation,charles law,boyles law etc...!
Kweli cacico hapa tatizo ni kutoweka mambo hadharani unatakiwa mwanamke akujue kabla hata hujamwoa, kama unajifanya mtu wa kujitutumua ku-solve matatizo ambayo huyawezi unategemea nini? au unajifanya upo njema mbele ya mpenzi wako unategemea nini hapo maana mkioana muda mwingi mpo wote lazima kila kitu kitajulikana, kweli jiamini kama alivyosema cacico
Kwahiyo Jodoki Kalimilo unamaanisha ni kweli tatizo lipo isipokuwa linasababishwa na wanaume wenyewe, yaani unakuta mwanaume anajifanya kuwa ana uwezo wa ku-solve matatizo ya mwenzi wake wakati kumbe uwezo huo hana isipokuwa ilikuwa njia tu ya kumpata
Sometime linasababishwa na wanaume kwa kushindwa kusema ukweli pale mizinga inapozidi lakini pia wakti mwingine pia kinadada kutokana na perception yao juu ya mwanaume flani kutokana na mwonekano wake na asset alizonazo unakuta mdada anaamini jamaa yupo njema kumbe mwisho wa siku anagundua hakuna kitu.
Kwahiyo gfsonwin tunaweza kusema wanaume wenye mtizamo niliouelezea ni wale ambao hawajakutana na wanawake waliopo kwenye hilo kundi lako la red, makes sense!
Inategemea elimu, utamaduni, dini, kabila.....wapo ambao ni wake kweli ukioa ni sawa umezaa mtoto ambaye kuanzia c...pi, hadi dawa ya mswaki ni lazima umnunulie.....lakini kuna wale ambao ni mwenza kweli, si mnyonyaji au anayetafuta mahali pa kuhemea. Kwa hiyo hatuwezi kugeneralize.