Eti wanawake 'wametakiwa' kuunga mkono rasimu ya Katiba!

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Hivi ni sahihi kusema 'wametakiwa'?! Au 'wameombwa'?! Halafu Sophia Simba na Celina Kombani ni akina nani 'kuwataka' badala ya 'kuwaomba' wanawake kupiga kura ya NDIO kupitishwa rasimu ya Katiba?!!

Halafu Celina anawaambia wanawake waache 'kubweteka', hivi ni kweli wanawake wamebweteka? Kule vijijini akina nani wako mstari wa mbele shambani? Mama ntilie mijini? Hivi yeye amefikaje hapo?!
CHANZO: ITV
 
Wanawake kwa miaka mingi wamekuwa wakidai haki zao za msingi zikiwemo haki za kupata nafasi sawa za uongozi, afya ya uzazi Salama, umri wa mtoto na mambo mengi ambayo yameshughulikiwa katika KATIBA inayopendekezwa. Kuhusu wanawake kutobweteka ni kweli wasimame I mara kiuchumi kwani ukijimudu kiuchumi ni rahisi kupata confidence ya kugombea nafasi za siasa kiuchumi na kijamii ktk Uongozi na kutoa mawazo. Lugha ya kuacha kubweteka Si ngeni Wala kebehi kwa wanawake tumeizoea. Wanawake tuipigie kura ya ndiyo KATIBA, tukisoma, tukaielewa itakuwa POWa kwetu
 
Sasa tatizo hapo nini? Watakiwe au waombwe suala la msingi hapo ni kuipigia kura katiba Pendekezwa kikubwa hapo waisome waielewe na siku ya mwisho waipigie kura ya ndiyo, haya mengine hayana mashiko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…