Mr Bluetooth
Senior Member
- Aug 23, 2022
- 123
- 230
Natumai mpo salama..
Nimeota ndoto nipo sehemu kama shuleni ama chuoni au mafunzoni nikawa ni mwanafunzi ninaefanya vizuri kiasi kwamba kuna mwalimu akawa ananipenda sana kama mwanafunzi wake bora, akawa ananiita tunakaa pembeni na ananifundisha mimi peke yangu lile suala kuna mwanafunzi mwenzangu akawa halipendi. Alichokifanya akaenda kwenye idara ya usalama kama vile polisi au takukuru kunisingizia kesi ya kutoa rushwa.
Siku nimekaa na mwalimu nawaona askari na watu wengine wakiambatana na yule mwanafunzi anaenichukia wamekuja kunikamata kwamba nina kesi ya kujibu, mara ghafla nikamuona mama angu mkubwa amekuja ananiambia nenda ukajibu tu mwanangu usiogope nikasema sawa naomba nikamuage mwalimu pale alipokaa.
Nikaenda kumuaga mwalimu nae akanipa maneno ya kunijaza ujasiri nisihofie huko wanakonipeleka nitarudi , nilivyorudi kwa wale watu waliokuja kunikamata nikamwambia yule mwanafunzi mwenzangu alienichongea kesi kwamba "jamaa nikirudi sitokuacha salama"
Wakati tunatoka mke wangu akawa amekuja eneo lile tukapishana nae tulivyofika nje kidogo nikaambiwa mkeo amefariki huko ndani alivyosikia umekamatwa, nikaanza kulia na nililia sana njia yote nakopitishwa kuelekea kituo cha polisi, nikiwa njiani nikawaona watu wawili mke na mume wake (hawa ni majirani) wamekaa wakiambizana 'yule analia mkewe amefariki' na wananiangalia bila hisia zozote yaani ni kama hawasikitishwi wala hawashangai ila wanaangalia tu yale yanayonitokea wakati huo mimi bado ninalia kwa kumpoteza mke wangu.
Ni nini maana ya hii ndoto?
NB: Ni kweli nimeoa.