Eti watanzania tunaongoza kwa kushangaa?

Eti watanzania tunaongoza kwa kushangaa?

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
542
Reaction score
735
Kwani likitokea tukio fulani lazima watu wajae kwa kulizunguka tukio huku wakishangaa na viminong'ono kidogo kidogo huku baadhi wakisikitika kwa kutingisha vichwa vyao, ila cha ajabu unaweza ukaenda kwenye hilo eneo lenye kundi la watu ukamuuliza mmoja wapo na akakujibu hajui kinachoendelea ingawa yupo eneo la tukio, yaan nae anashangaa na ww unajiunga kushangaa bila kujua chochote, ni mwendo wa kushangaaa shangaa tu ukipita mijini huko utakuta vikundi vikundi vikishaangaa matukio tofauti tofauti mara waganga wakionyesha madawa yao yanavyotibu nguvu za kiume, kule mwizi kapigwa kachakaa mara huku wengine wakishangaa picha kwenye magazeti na wengine wakiwashangaa wamachinga wanaonadisha bidhaa zao yaani ni full kushangaa shangaa...

Sasa najiuliza hivi inawezekana sisi wana wa Tanganyika tukawa tunaongoza kushangaa shangaa?
IMG-20190529-WA0007.jpg
 
Back
Top Bottom