Etiene Ndairagije apewa mikoba ya kuinoa taifa stars

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Aliyekuwa kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars,Mrundi Etienne Ndairagije amepewa mkataba wa mwaka mmoja kuinoa timu ya taifa ya Tanzania,taarifa iliyotoka jioni hii kutoka ndani ya TFF imethibitisha kuwa kocha Ndairagije atakuwa kocha mkuu wa Tanzania.

Ndairagije ambaye mwanzoni mwa week hii aliacha rasmi na Azam Fc kwa makubaliano maalum amepewa jukumu hilo baada ya kuiwezesha Tz kufuzu michuano inayoshirikisha wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN nchini Cameroon.

Je atatuvusha au alibahatisha tu?

Kila la heri Ndairagije Etiene
 
Msaidizi wake Matola nae imekuaje?
 
Hongera Etienne Ndairagije , kila la heri kuwa jasirina Mvumilivu. Taifa Stars ni pasua Kichwa!
 
Mwaka mmoja? Ili afanye nn kwa huo mda mfupi. Only in bongo.
 
Aongeze sasa nguvu kwenye zile beki zake za pembeni, upande wa kulia. Shomari Kapombe, Paul Godfrey au Juma Abdul hawakwepeki.

Kuwang'ang'ania Boniface Maganga, Haruna Shamte na Salum Kimenya, kutaendelea kutengeneza uchochoro usio na ulazima.
 
Uzuri wa huyu kocha ni msikivu na anashirikiana vyema na wasaidizi wake, pia mwepesi kukubali kasoro zinazoonekana kwenye uwanja na sio kukumbatia wachezaji mizigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…