Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kampuni za Pfizer-BioNTech na Moderna ziliongeza bei zao za chanjo ya corona katika makubaliano ya hivi karibuni na Jumuiya ya Ulaya (EU).
Kulingana na Financial Times, bei ya dozi 1 ya chanjo ya Pfizer-BioNTech iliongezeka kutoka euro 15.50 hadi euro 19.50.
Bei ya dozi moja ya Moderna, ambayo ilikuwa karibu dola 22.60 hapo awali, ilipanda hadi kufikia karibu dola 25.50 katika mkataba mpya.
Ikitangaza kuwa imefikia lengo lake la chanjo ya asilimia 70 ya idadi ya watu wazima mnamo Julai 27, EU inapanga kununua zaidi ya dozi bilioni 1 za chanjo mwishoni mwa Septemba.
Wakala wa Dawa za Ulaya (EMA) inaruhusu matumizi ya chanjo zinazozalishwa na kampuni za Pfizer-BioNTech, Moderna, AstraZeneca na kampuni za Johnson and Johnson katika nchi za EU hadi sasa. EMA inaendelea tathmini ya awali ya chanjo ya Sinovac, Curevac, Novavax, Sputnik V na Sanofi Pasteur.