EURO2020: England VS Italia | Je, wajua England imeshinda mara moja tu dhidi ya Italia ikiwa Wembley?

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Fainali hii inayofanyika katika Dimba la Wembley huko London, Uingereza inawaleta pamoja Italia inayoangalia namna ya kuongeza taji jingine la EURO baada ya ya miaka 53 na England inayoangazia namna ya kuchukua taji lake la kwanza la michuano hiyo

Italia imeshapoteza fainali mbili tangu ishinde taji hilo mara ya mwisho huko Rome mwaka 1968 huku England ikiingia fainali kwa mara ya kwanza baada ya kutolewa kwenye hatua ya nusu fainali mara mbili ilizoingia mwaka 1968 - huko Italia na 1996 ikiwa mwenyeji

Itakumbukwa kuwa timu zote zilihitaji muda wa nyongeza (dakika 120) katika michezo yao ya nusu fainali ili kuingia fainali ambapo Italia iliitoa Uhispania (Bingwa mara 3) kwa penati baada ya droo ya goli 1-1, huku England ikiitoa Denmark kwenye dakika hizo za nyongeza

Timu tatu tu zimeshinda taji hilo zikiwa kama mwenyeji Uhispania (1964), Italia (1968) na Ufaransa (1984). Ureno (2004) na Ufaransa (2016) ziliingia fainali lakini hazikufanikiwa kuchukua taji hilo.


Je, timu hizi zilivyokutana huko nyuma ilikuwaje?

Timu hizi zimekutana mara chache katika miaka miaka mingi, Italia imeshinda michezo 10 katika 27 iliyokutana na England, huku England ikishinda michezo 8. Hata hivyo England imefunga magoli mengi 33, mawili zaidi ya Azzurri

Mchezo wa karibuni zilipokutana timu hizo ilikuwa mwaka Mei 2018 katika mchezo wa kirafiki, pale Wembley ambapo timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1. Penati ya Lorenzo Insigne katika dakika ya 87 ikisawazidha goli la Jamie Vardy (26').

Mchezo wa mwisho wa kimashindano baina ya timu hizo ulikuwa mwaka 2014 katika mchezo wa makundi ya Kombe la Dunia huko Manaus ambapo Italia iliibuka na ushindi wa goli 2-1.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu hizo kukutana katika EURO tangu zilipokutana katika michuano hiyo mwaka 2012 katika mchezo wa robo fainali huko Kyiv. Italia iliibuka na ushindi wa penati 4-2 baada ya timu hizo kwenda sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120

England haijashinda dhidi ya Italia kwenye michezo 6 ya michuano mbalimbali iliyokutana (D2 L4), tangu ipate ushindi wa goli 2-0 katika kampeni za kufuzu kucheza Kombe la dunia 1978.

Ushindi wa goli 2-0 walioupata England November 1977 ni ushindi pekee walioupata dhidi ya Azzurri katika mechi 6 zilizochezwa Wembley (D3 L2).

FAHAMU REKODI YA TIMU HIZI KATIKA UPIGAJI PENATI


Rekodi ya Italia katika upigaji penati kwenye michuano mikubwa kwa sasa ni W5 L7:
8-9 v Czechoslovakia, 1980 UEFA European Championship third-place play-off
3-4 v Argentina, 1990 FIFA World Cup semi-final
2-3 v Brazil, 1994 FIFA World Cup final
3-4 v France, 1998 FIFA World Cup quarter-final
3-1 v Netherlands, UEFA EURO 2000 semi-final
5-3 v France, 2006 FIFA World Cup final
2-4 v Spain, UEFA EURO 2008 quarter-final
4-2 v England, UEFA EURO 2012 quarter-final
6-7 v Spain, 2013 FIFA Confederations Cup semi-final
3-2 v Uruguay, 2013 FIFA Confederations Cup third-place play-off
5-6 v Germany, UEFA EURO 2016 quarter-final
4-2 v Spain, UEFA EURO 2020 semi-final

Rekodi ya England kwenye upigaji penati kwa sasa kwenye michuano mikubwa ni W3 L6,
3-4 v West Germany, 1990 FIFA World Cup semi-final
4-2 v Spain, EURO '96 quarter-final
5-6 v Germany, EURO '96 semi-final
3-4 v Argentina, 1998 FIFA World Cup round of 16
5-6 v Portugal, UEFA EURO 2004 quarter-final
1-3 v Portugal, 2006 FIFA World Cup quarter-final
2-4 v Italy, UEFA EURO 2012 quarter-final
4-3 v Colombia, 2018 FIFA World Cup round of 16
6-5 v Switzerland, 2019 UEFA Nations League third-place play-off

Hakuna Timu iliyowahi kushinda katika upigaji wa penati mara 2 katika shindano moja la EURO
 
Ukiangalia walikotoka, unaona kabisa Italy wako vizuri zaidi ya England! Kitakacho wabeba Waingereza ni home advantage tu, hakuna kingine.

All in all, naipa nafasi Italia! Kiukweli wamekamilika kila idara. Na hawana mambo ya kitoto kitoto ya kujirusha ndani ya 18 kama akina Rahim Sterling.
 
Italy wasicheze tuu kama walivyocheza na Spain ,hawatatoboa !
 
Italy wasicheze tuu kama walivyocheza na Spain ,hawatatoboa !
Wamecheza vile na Spain kwavile mpira wa Spain ni wa Tiktak hivyo ni lazima wacheze kwa mbinu ya kujilinda na kucheza counter attack na aliyeharibu mashambulizi ni Immobile wanapopiga counter. Pia pengo la spinazzola limeonekana sana maana ndiye mchezaji alioko nyuma mwenye uwezo wa kukaba pamoja na kupeleka mashambulizi kwa kasi. Kulikuwa na uelewano mzuri sana pale nyuma pamoja na viungo. Lakini aliyechukua nafasi yake anashindwa kuvivaa viatu vya spinazzola.
 
Tarehe 11/07/2021 england itashinda kwa mara ya pili dhidi ya italy katika dimba la wembley
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…