Evance Aveva Afungwa kifungo cha nje, Kaburu aachiwa huru

Evance Aveva Afungwa kifungo cha nje, Kaburu aachiwa huru

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hivi ndivyo walivyohukumiwa na Mahakama siku ya Leo, Aveva amefungwa kifungo cha nje cha miezi 6 kwa matumizi mabaya ya ofisi, huku Kaburu akiachiwa huru kwa kuonekana hana hatia.

======

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Rais wa Simba, Evans Aveva kifungo cha nje miezi sita kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi huku Godfrey Nyange maarufu Kaburu akiachiwa huru baada ya mahakama hiyo kutomkuta na hatia.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba leo Alhamisi Oktoba 28,2021 amesema hakuna ubishi wowote Dola za kimarekani 300,000 zilikuwa zimeingizwa kwenye akaunti ya Klabu ya Simba kupitia benki ya CRDB ambayo ni mauzo ya mchezaji Emanuel Okwi.

Amesema baada ya kuingia kwenye akaunti inaonyesha kamati tendaji ya klabu hiyo ilielekeza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti ya Simba ili zitumike kujenga nyasi bandia katika Uwanja wa Bunju.

"Mahakama imejitosheleza Kuwa Ile fedha ilitakiwa ijenge nyasi bandia kwenye uwanja wa Bunju lakini haikufanyika hivyo matokeo yake zilienda kwenye akaunti binafsi ya Aveva,"amesema Thomas Simba.

Mahakama hiyo imejiridhisha kuwa mashtaka yote hayajadhibitishwa, isipokuwa shtaka la matumizi mabaya ya ofisi ambayo ni kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Klabu ya Simba kwenda akaunti binafsi.

Simba amesema kutokana na mashtaka hayo Nyange amekutwa hana hatia na Aveva amekutwa na hatia Kwa kutumia nafasi yake vibaya kwa Kuingiza fedha hizo kwenye akaunti binafsi ingawa hakuna wizi uliofanyika.

"Hela zote zilitumika kihalali isipokuwa tatizo lake hizo fedha ziliingizwa kwenye akaunti binafsi” amesema Simba
Wakili wa Serikali, Fatima Waziri amedai hawana kumbukumbu ya makosa ya jinai yaliyotendwa na mshtakiwa huyo, hivyo aliiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe funzo kwake na kwa wengine wanaotumia madaraka vibaya ya ofisi.

Wakili wa utetezi, Kuge Wabeya aliieleza mahakama hiyo kuwa kosa hilo ni la Kwanza pia mshtakiwa huyo ni mgonjwa amekuwa akihudhuria kliniki mara tatu kwa wiki na ana familia inayomtegemea.

Hakimu Simba amesema kutokana na mazingira yaliyopo ya kesi amezingatia hoja za pande zote mbili
"Kumpeleka gerezani Kwa maana kumfunga haitasaidia chochote kwani watakuwa wamemfunga mgonjwa ambaye utakuwa imesababisha usumbufu siyo Kwa mshtakiwa bali hata magereza na jamii Kwa ujumla,"amesema Simba.

"Hata ukimpiga faini kubwa bado haitasaidia chochote kwani asipolipa atalazimika kupelekwa gerezani hivyo adhabu pekee inayomfaa mahakama imeona atumikie kifungo cha nje miezi Sita na asifanye kosa lolote,"amesema.

Simba alisema rufaa ipo wazi kwa yeyote hajaridhika na maamuzi hayo

Katika kesi ya msingi Aveva wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Kimarekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Chanzo: Mwananchi
 
Hii Simba bila;
Kaburu
Aveva
Hanspop
Michael Wambura
Tulli
Manara et al
Ndio maaana tunapigwa na Waporipori ovyo ovyo maaana timu haina watoto wa Mjini. Mpira somtime ni mchezo unataka swagga za Kihuni ili utoboe ndio maaana Utto waliwarudisha lile genge la Mafia wao watatu.
 
Hii Simba bila;
Kaburu
Aveva
Hanspop
Michael Wambura
Tulli
Manara et al
Ndio maaana tunapigwa na Waporipori ovyo ovyo maaana timu haina watoto wa Mjini. Mpira somtime ni mchezo unataka swagga za Kihuni ili utoboe ndio maaana Utto waliwarudisha lile genge la Mafia wao watatu.
Acha ujinga wewe,,, wakati simba inachukua ubingwa mara nne mfululizo na robo fainali Africa champion league hao kina aveva walikuwepo? Au wewe ndo aveva umetoka jela leo na kujipigia promo humu
 
wamemfungia nini sasa, hiyo ofisi yenyewe iko wapi

hopeless
 
Acha ujinga wewe,,, wakati simba inachukua ubingwa mara nne mfululizo na robo fainali Africa champion league hao kina aveva walikuwepo? Au wewe ndo aveva umetoka jela leo na kujipigia promo humu
Wewe kweli mporipori wa matombo ndani ndani huko. Unamjua Hanspop wewe?? Nyerere alimshindwa yule kiumbe ijje kuwa hawa Utopolo. Msiba wa Hanspop unajua umeacha pengo gani mama-eeee zako hujui umafia wa mpira kaaa kimia
 
Wewe kweli mporipori wa matombo ndani ndani huko. Unamjua Hanspop wewe?? Nyerere alimshindwa yule kiumbe ijje kuwa hawa Utopolo. Msiba wa Hanspop unajua umeacha pengo gani mama-eeee zako hujui umafia wa mpira kaaa kimia
Zilongwa mbali zitendwa mbali,,, hebu rudia kusoma hiyo coment yangu,, kwa maana tunajua kabisa wote kama hanspope amefariki na alikuwepo kipindi ambacho simba inachukua ubingwa mara nne mfululizo,,, huyo wambura,aveva, kaburu hao matapeli tu,, na kipindi chao walifanya nini zaidi upigaji tu,,
Alafu leo eti useme simba bila wao kwa kuwa watoto wa mjini basi mambo hayaendi, kwani mji mzima simba watoto wa mjini wako wao tu!,, na hiyo miaka ya nyuma wakati simba inachukua ubingwa wao walikuwepo? Alafu unajidai we town labda town ya mvuti
 
Dah! Yaani mpaka watu wanahukumiwa vifungo kwa kununua nyasi bandia kwa ajili ya uwanja wao huko Bunju, leo hii uwanja wenyewe eti unaitwa Mo Arena!!

Bora hata ungeitwa HAssan Dalali Bunju Compex, ili kumuenzi huyu Mzee asiye na elimu ya darasani, lakini aliyekuwa na maono ya mbali kwa klabu yake ya simba ukilinganisha na huyu mdhamini wao janja janja.
 
Kaburu inafaa apewe nafasi, kina mula ngambi wapi pale kwa faida yao hata kusajili wachezaji hawawezi. Kina magori wanalialia Kuna usaliti wakati Mangungu no mwenyekiti jina
 
Back
Top Bottom